AU yapongeza mfumokazi wa Doha ikiuelezea kuwa ni ‘hatua muhimu’ kutatua mgogoro kati ya DRC na M23

(CRI Online) Novemba 18, 2025

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf amekaribisha kusainiwa kwa mfumokazi wa Doha kwa ajili ya makubaliano ya kina ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la M23 nchini Qatar.

Taarifa iliyotolewa na Umoja huo Jumamosi iliyopita imesema, hatua hiyo muhimu inawakilisha upigaji hatua mkubwa kuelekea kurejesha utulivu, kujenga upya kuaminiana, na kushughulikia chanzo cha mgogoro huo wa mashariki mwa DRC.

Akizipongeza pande hizo mbili kwa kuonyesha ujasiri, utayari wa kisiasa, na dhamira kwa majadiliano, Youssouf pia ameeleza shukrani zake kwa Qatar kwa uwezeshaji wa kiujenzi na uungaji wake mkono kwenye mchakato huo wa amani.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha