Lugha Nyingine
Upandaji wa miparachichi wastawi katika Wilaya ya Menglian, Kusini-Magharibi mwa China

Mwanamke akiuza parachichi kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni kwenye kampuni katika Wilaya ya Menglian ya Mji wa Pu'er, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Novemba 16, 2025. (Picha na Liang Zhiqiang/Xinhua)
Miti ya matunda ya Parachichi hustawi katika mazingira yenye mwanga wa kutosha wa jua na halijoto inayofaa, na hapo kabla, parachichi zilizokuwa zikiuzwa nchini China zaidi zilikuwa zile zilizoagizwa kutoka nchi zingine.
Lakini hivi sasa hali imekuwa tofauti, kwani Wilaya ya Menglian katika Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China iliyopo kwenye latitudo sawa na nchi ya Mexico inayozalisha parachichi kwa wingi duniani, imekuwa ni moja ya maeneo machache nchini China yanayopanda miparachichi mingi na kuzalisha parachichi zenye ubora wa juu.
Tangu ilipoanza kupanda miparachichi kwa mara ya kwanza mwaka 2007, wilaya hiyo ya Menglian kwa sasa imekuwa moja ya maeneo yanayozalisha parachichi kwa wingi nchini China, na eneo lake la jumla la kupanda miparachichi limefikia ukubwa wa hekta zaidi ya 8,000.

Wafanyakazi wakielezea hali ya uzalishaji wa parachichi kwenye karakana ya kampuni ya kupanda miparachichi katika Wilaya ya Menglian ya Mji wa Pu'er, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Novemba 16, 2025. (Picha na Liang Zhiqiang/Xinhua)

Mfanyakazi akipanga midoli yenye umbo la parachichi kwenye hoteli katika Wilaya ya Menglian ya Mji wa Pu'er, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Novemba 18, 2025. (Picha na Liang Zhiqiang/Xinhua)

Mfanyakazi akimimina kahawa ya parachichi kwenye kampuni katika Wilaya ya Menglian ya Mji wa Pu'er, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Novemba 17, 2025. (Picha na Liang Zhiqiang/Xinhua)

Mwanakijiji akivuna parachichi kwenye shamba la kupandwa kwa miparachichi katika Wilaya ya Menglian ya Mji wa Pu'er, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Novemba 16, 2025. (Picha na Liang Zhiqiang/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



