Balozi wa China nchini Zambia asema Uhusiano kati ya China na Zambia ni mfano mzuri wa ushirikiano wa Kusini-Kusini

(CRI Online) Novemba 19, 2025

Balozi wa China nchini Zambia Han Jing amesema uhusiano kati ya China na Zambia unaenda mbali zaidi ya wigo wa uhusiano wa pande mbili na kuwa alama ya urafiki kati ya China na Afrika na mfano wa ushirikiano wa Kusini-Kusini.

Balozi Han ametoa kauli hiyo Jumamosi kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua. Amesema kupandishwa kwa hadhi ya uhusiano wa pande mbili kati ya China na Zambia kuwa uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote mwaka 2023 kumefungua maeneo mengine ya ushirikiano na kuimarisha uratibu kati ya pande hizo.

Balozi Han amezungumzia miradi kadhaa mikubwa ya pamoja ambayo imepiga hatua vizuri, kama vile kuzinduliwa kwa mradi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Jua wa Chisamba na Mgodi wa Shaba wa Lubambe.

"Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imeendelea kuwa alama kubwa ya urafiki kati ya China na Afrika," Balozi Han amesema, akiongeza kuwa mpango wake wa kuifufua utaimarisha muunganisho wa kikanda wa Zambia na kuunga mkono azma yake ya kuwa "nchi iliyounganishwa na ardhi" na kitovu cha viwanda cha kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha