China yasema Japan haina sifa kabisa za kutafuta nafasi ya kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 19, 2025

Fu Cong, mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, akizungumza kwenye mjadala wa mwaka huu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya mageuzi ya Baraza la Usalama, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Novemba 18, 2025. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA – Kauli za Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi juu ya Taiwan ni za makosa makubwa na hatari sana, Fu Cong, mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amesema jana Jumanne, akiongeza kuwa kauli hizo zinaingilia kati kwa kiasi kikubwa mambo ya ndani ya China.

"Kauli hizo zinaingilia kati kwa kiasi kikubwa mambo ya ndani ya China na zinakiuka sana kanuni ya kuwepo kwa China moja na moyo wa nyaraka nne za kisiasa kati ya China na Japan," Fu amesema kwenye mjadala wa mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya mageuzi ya Baraza la Usalama.

Amesema kauli kama hizo ni dhihaka kwa haki ya kimataifa, utaratibu wa kimataifa wa baada ya vita vya Pili vya Dunia, na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa, na zinakwenda kinyume na ahadi ya Japan ya maendeleo ya amani.

"Nchi kama hiyo haina sifa kabisa za kutafuta nafasi ya kudumu kwenye Baraza la Usalama," ameongeza.

Fu Cong, mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, akizungumza kwenye mjadala wa mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya mageuzi ya Baraza la Usalama, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Novemba 18, 2025. (Xinhua/Xie E)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha