Waziri Mkuu wa China asema SCO inaweza kubeba jukumu kubwa zaidi katika kuhimiza usimamizi bora duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 19, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Moscow, Russia, Novemba 18, 2025. (Xinhua/Gao Jie)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Moscow, Russia, Novemba 18, 2025. (Xinhua/Gao Jie)

MOSCOW - Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ina zana na uwezo wa kutekeleza kwa pamoja wa Pendekezo la Usimamizi Duniani (GGI) kama fursa ya kubeba jukumu kubwa zaidi katika kuileta dunia usimamizi bora, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema jana Jumanne alipokuwa akihutubia Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa SCO ambao uliongozwa na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin mjini Moscow.

“Rais Xi Jinping wa China alipendekeza kwa dhati GGI kwenye Mkutano wa Viongozi wa SCO wa Tianjin mwezi Septemba, akitoa hekima na suluhu za China ili kusaidia jumuiya ya kimataifa kwa pamoja kukabiliana mageuzi duniani na changamoto za dharura,” Li amesema.

Amesisitiza umuhimu wa SCO katika kujenga na kuufanyia mageuzi mfumo wa usimamizi duniani.

“Kwanza, SCO inapaswa kutumia kikamilifu nguvu zake bora za kipekee,” Li amesema.

Akitaja kuwa Moyo wa Shanghai unaendana sana na dhana kuu za GGI, Li amesema kuwa SCO ina uzoefu mkubwa wa kivitendo na dhamana thabiti za kiutendaji, na inapaswa kutumia kikamilifu faida hizo bora kutoa mchango zaidi kwa usimamizi duniani na kusaidia kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

“Pili, SCO inapaswa kutilia maanani katika maeneo muhimu ya maendeleo na usalama,” amesema.

Ametoa wito kwa nchi wanachama wa SCO kuhimiza maendeleo na usalama kupitia ushirikiano, kuongeza kuendana kwa mikakati ya maendeleo, kuhimiza ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuhakikisha utulivu na ufanisi wa mnyororo wa viwanda na usambazaji bidhaa duniani, na kwa pamoja kujenga uchumi wa dunia ulio wazi na jumuishi.

“Tatu, SCO inapaswa kuchochea nguvu kubwa kwa ajili ya uvumbuzi na mageuzi,” amesema, huku akihimiza pande zote kuimarisha ushirikiano katika sayansi na teknolojia pamoja na uvumbuzi wa kiviwanda, na kuhimiza ushirikiano katika nishati ya jadi na nishati mbadala.

Li amesema kwamba viongozi katika Mkutano wa kilele wa SCO wa Tianjin kwa pamoja walipitisha mkakati wa maendeleo kwa ajili ya SCO katika kipindi cha 2026-2035.

Amesema China inapenda kushirikiana na nchi zote wanachama ili kuimarisha zaidi uratibu wa kimkakati, kuhimiza kwa ufanisi utekelezaji wa ushirikiano, kuboresha mfumo wa uendeshaji, kuongeza zaidi mshikamano, uwezo wa utekelezaji na ushawishi, na kuifanya SCO kuwa bora na imara zaidi.

Washiriki wengine waliohudhuria mkutano huo wamesema kuwa SCO inabeba jukumu muhimu linalozidi kuongezeka katika kuhimiza mafungamano ya kikanda na kuwezesha kuanzishwa kwa dunia yenye ncha nyingi ya haki na usawa.

Wametoa wito kwa pande zote kushirikiana kutekeleza matokeo ya Mkutano wa Viongozi wa SCO wa Tianjin, kuboresha mfumo wa jumuiya, kuendana na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutekeleza mkakati wa maendeleo wa SCO kwa ajili ya kipindi cha 2026-2035. 

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha