Kenya yaweka tahadhari ya juu baada ya mlipuko wa virusi vya Marburg nchini Ethiopia

(CRI Online) Novemba 19, 2025

Kenya imesema mamlaka zake za afya ziko katika hali ya tahadhari ya juu kufuatia vifo vya watu watatu vinavyohusiana na ugonjwa wa virusi vya Marburg katika nchi jirani ya Ethiopia.

Taasisi ya Afya ya Umma ya Kenya (KNPHI) imesema katika taarifa yake ya jana Jumanne kwamba ingawa Kenya haijaripoti kesi zozote za ugonjwa huo, nchi hiyo inaendelea kuwa katika hali ya tahadhari ya juu kutokana na shughuli nyingi za kuvuka mpaka kutoka Ethiopia kupitia viwanja vya ndege vya kimataifa na mipaka ya ardhini, ikifanya hatari ya virusi hivyo kuwa yenye umuhimu wa kufuatiliwa katika afya ya umma ya nchi hiyo.

Taasisi hiyo imezishauri kaunti kutoa elimu kwa wahudumu wa afya kuhusu ufahamu wa kina wa ugonjwa huo, na kuimarisha ufuatiliaji katika maeneo ya mpakani, vituo vya afya, na katika jamii ili kugundua kwa haraka na kuripoti kesi zinazoshukiwa kuwa za ugonjwa huo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha