Miundombinu ya kuchajia magari yanayotumia umeme ya China yaonesha ukuaji dhahiri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2025

Magari yanayotumia umeme yakiwa yanachajiwa kwenye kituo cha Bustani ya Quanhu cha kuchaji kwa haraka sana majimaji yanayopozwa mjini Guiyang, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Juni 13, 2025. (Xinhua)

Magari yanayotumia umeme yakiwa yanachajiwa kwenye kituo cha Bustani ya Quanhu cha kuchaji kwa haraka sana majimaji yanayopozwa mjini Guiyang, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Juni 13, 2025. (Xinhua)

BEIJING – Takwimu zilizotolewa na idara husika ya kiserikali ya China jana Jumatano zinaonesha kuwa, idadi ya vituo vya kuchajia magari yanayotumia umeme (EV) nchini China ilifikia zaidi ya milioni 18.64 hadi kufikia mwishoni mwa Oktoba mwaka huu, imefikia ongezeko la asilimia 54 kuliko mwaka mmoja uliopita.

Kati yao, milioni karibu 4.53 vilikuwa vituo vya kuchajia vya kiumma, zaidi ya milioni 14.11 ni vituo vya kibinafsi, ambavyo vimefikia ongezeko la asilimia 39.5 na asilimia 59.4, mtawalia, takwimu hizo zinaonyesha.

Kulingana na takwimu hizo, nguvu ya pamoja ya vituo hivyo vya kuchajia magari yanayotumia umeme vya kiumma ilikuwa kilowati takriban milioni 203 mwishoni mwa Oktoba, au kilowati 44.69 kwa wastani.

Mapema mwezi uliopita, China ilitangaza kwa umma mpango utekelezaji wa miaka mitatu wa kuboresha miundombinu ya kuchajia magari yanayotumia umeme ya kote nchini ikilenga kuanzisha mtandao wa vituo vya kuchajia milioni 28, huku uwezo wa vituo vya kuchajia vya kiumma ukiwa umepangwa kuzidi kilowati milioni 300 itakapofika mwishoni mwa mwaka 2027.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha