Lugha Nyingine
Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya China Bara akosoa maneno ya uchochezi aliyosema Waziri Mkuu wa Japan kuhusu Taiwan

Zhu Fenglian, Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, akionyesha ishara kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, China, Novemba 19, 2025. (Xinhua/Pan Xu)
BEIJING - Zhu Fenglian, Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China amesema maneno ya uchochezi aliyosema hivi karibuni Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi kuhusu Taiwan yanakanyaga haki ya kimataifa, yanapinga utaratibu wa kimataifa wa baada ya Vita vya Pili vya Dunia, na yanaharibu vibaya uhusiano kati ya China na Japan.
Zhu alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatano kwamba maneno hayo aliyosema Takaichi yanajaribu kuingilia kati hali ya mambo ya Mlango-Bahari wa Taiwan, kutotambua matokeo ya Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan, na kufufua nguvu ya umilitalizm.
"Maneno yake hayo bila shaka yanasababisha malalamiko na ufuatiliaji mkubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa," Zhu amesema.
Amesisitiza kwamba suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya China na uingiliaji kati wowote wa nje hauvumiliki, akihimiza Japan kuacha mara moja kuingilia mambo ya ndani ya China, kusitisha uchochezi wake, na kujizuia kwenda mbali zaidi katika njia potofu.
"Tunatumai ndugu wa Taiwan watatambua hali ya hatari na madhara ya vitendo husika vya Japan, kujiunga pamoja nasi katika kuangamiza kithabiti shughuli zote za mafarakano zinazolenga 'kujitenga kwa Taiwan' na uingiliaji wote wa nje, na kulinda nchi yetu ya pamoja ya Taifa la China," Zhu amesema.
Akijibu kuhusu kitendo cha Lai Ching-te kuunga mkono na kuitikia maneno ya Takaichi, Zhu amesema kwamba chanzo kikuu cha hali wasiwasi katika Mlango-Bahari wa Taiwan ni ukaidi wa utawala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (DPP) kushikilia msimamo wa mafarakano wa kutaka "Taiwan Ijitenge" na kushirikiana kishoga na nguvu za nje ili kutafuta kujitenga.
Vyombo vingi vya habari, wataalamu, na wasomi wa nje hivi karibuni wamekosoa utawala wa DPP kwa hatua zao zisizofikiriwa kwa busara , wakiwaita kuwa ni "waharibifu wa amani na waleta matata katika Mlango Bahari wa Taiwan".
Ameuonya vikali utawala wa DPP kwamba kutegemea nguvu za nje kutafuta kujitenga si chochote bali ni udanganyifu mtupu, na yeyote anayesahau asili yake na kusaliti taifa atalaumiwa na historia.

Zhu Fenglian, Msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, akionyesha ishara kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, China, Novemba 19, 2025. (Xinhua/Pan Xu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



