Waziri Mkuu wa China asema China yapenda kushirikiana na Zambia na Tanzania kujenga kituo kipya cha uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akizungumza kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kufufua Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mjini Lusaka, Zambia, Novemba 20, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akizungumza kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kufufua Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mjini Lusaka, Zambia, Novemba 20, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

LUSAKA - Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Alhamisi wakati akihudhuria hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kufufua Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) pamoja na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia na Makamu Rais wa Tanzania Emmanuel Nchimbi katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, amesema kwamba China inapenda kushirikiana na Zambia na Tanzania ili kusukuma mbele maendeleo ya ukanda wa ustawi kando ya reli hiyo ya TAZARA, na kujenga kwa pamoja kituo kipya cha ukuaji wa uchumi.

Waziri Mkuu Li amesema kwamba mwezi Septemba 2024, Rais Xi Jinping wa China, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais Hichilema wa Zambia walishuhudia kwa pamoja kusainiwa kwa makubaliano ya maelewano (MoU) kuhusu mradi huo wa kufufua Reli ya TAZARA mjini Beijing.

"Katika kipindi cha mmoja mwaka uliopita, idara na kampuni husika za nchi hizo tatu zimefanya kazi kwa umoja na kuchukua hatua madhubuti ili kupiga hatua muhimu, zikiandaa njia kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mradi huo," Waziri Mkuu Li amebainisha.

"Reli hiyo inaunganisha watu wa China, Tanzania na Zambia kwa karibu," amesema, akisifu moyo wa TAZARA kuwa ni urithi wa thamani uliojengwa kwa kujitolea na kazi ngumu -- ambao unapaswa kuthaminiwa na kulindwa.

Waziri Mkuu Li amesema, leo, ushirikiano kati ya China na Afrika umeanza safari mpya ya kuelekea ndoto ya pamoja ya ujenzi wa mambo ya kisasa wakati huohuo akiielezea reli hiyo kuwa ni mradi kinara wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

"China inapenda kushirikiana na Zambia na Tanzania ili kuhakikisha kwamba reli hii, iliyojaa matumaini, inang'aa kwa uzuri mpya katika zama mpya, na kuingiza nguvu hai zaidi katika maendeleo ya Tanzania na Zambia, na hata Afrika nzima," amesema.

Ametoa wito kwa nchi hizo tatu kuchukua mradi huo wa ufufukaji wa reli hiyo kama fursa ya kusukuma mbele muunganisho wa miundombinu kama vile reli, barabara kuu na bandari, na kuimarisha muunganisho katika nyanja zikiwemo za forodha, ukaguzi wa bidhaa na mambo ya ushuru.

Kwa upande wao, Hichilema na Nchimbi wamesema kwamba reli hiyo ni ukumbusho wa urafiki uliojengwa na vizazi vya zamani vya viongozi wa nchi hizo tatu, na pia ni ishara ya jitihada za watu wao kutafuta uhuru, kujitegemea, mshikamano na kuungana mkono.

“Kufufua reli hii kunaonyesha mustakabali wa pamoja wa mataifa haya matatu na juhudi zao za pamoja za kujenga mustakabali mzuri,” wamesema, wakiongeza kuwa reli hiyo itakuwa mfano wa namna watu wa China na Afrika wanavyorithisha urafiki wao na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya ufufuaji.

Kwenye hafla hiyo, serikali za China, Tanzania na Zambia zimetoa taarifa ya pamoja kuhusu ujenzi wa pamoja wa ukanda wa ustawi wa Reli ya TAZARA.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kufufua Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) pamoja na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia na Makamu Rais wa Tanzania Emmanuel Nchimbi mjini Lusaka, Zambia, Novemba 20, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kufufua Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) pamoja na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia na Makamu Rais wa Tanzania Emmanuel Nchimbi mjini Lusaka, Zambia, Novemba 20, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha