Rais Xi Jinping atoa maelekezo muhimu juu ya kuhimiza kikamilifu utawala wa sheria

(CRI Online) Novemba 21, 2025

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) hivi karibuni ametoa maelekezo muhimu kuhusu kusukuma mbele kikamilifu utawala wa sheria.

Amebainisha kuwa tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike, Kamati Kuu ya CPC imejumuisha kwa juhudi ya kusukuma mbele utawala wa sheria kwenye mpango mkakati wa “Vifungu Vinne” na kuuendeleza kwa nguvu.

Amesema, kutokana na juhudi hizo, mfumokazi kwa ajili ya utawala wenye msingi wa sheria kikamilifu umeundwa, mfumo wa utawala wa sheria wa kijamaa wenye umaalum wa China umekuwa ukiboreshwa kila wakati, na njia ya utawala wa sheria wa kijamaa wenye umaalum wa China imepanuliwa kwa kasi tulivu.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha