Kundi la M23 lasema mazungumzo ya amani na serikali ya DRC kuendelea Doha

(CRI Online) Novemba 21, 2025

Kundi la waasi la M23 limesema kuwa majadiliano na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yanatarajiwa kuendelea katika mji wa Doha, Qatar katika wiki zijazo kufuatia kusainiwa kwa mfumokazi wa makubaliano kwa ajili ya amani kati ya pande hizo mbili.

Wakizungumza jana Alhamisi mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini ambao unashikiliwa na M23, maofisa wa kundi hilo wamesema mazungumzo hayo yatalenga masuala muhimu kama njia za kupitisha misaada ya kibinadamu, uhakika wa kisheria, na namna ya kuachia wafungwa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha