Moto wasababisha watu kuondolewa kwenye ukumbi wa Mkutano wa COP30 nchini Brazil

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2025

Wafanyakazi wa usalama wakidhibiti njia ya kuingia ndani ya ukumbi wa Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP30) baada ya moto kuzuka mjini Belem, Jimbo la Para, Brazil, Novemba 20, 2025. (Picha na Lucio Tavora/Xinhua)

BELEM - Moto ulizuka jana Alhamisi kwenye moja ya kumbi za Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP30) unaoendelea katika Mji wa Belem nchini Brazil, na kusababisha watu kuondolewa na idara ya zimamoto, kwa mujibu wa taarifa kutoka mamlaka za serikali ya Brazil.

“Tukio hilo limetokea kwenye Eneo la Bluu, eneo ambalo lina mabanda ya kimataifa na vyumba vilivyowekwa kwa ajili ya mazungumzo rasmi,” wamesema waandaaji wa mkutano huo.

Waziri wa Utalii wa Brazil Celso Sabino amesema kwamba moto huo, ambao ulizuka muda mfupi baada ya saa 8 mchana kwa saa za Brazil, ulikuwa umeshadhibitiwa ilipofika muda wa karibu saa 8:30 mchana, huku kukiwa hakuna majeruhi yoyote yaliyoripotiwa hadi sasa.

Helder Barbalho, Gavana wa Jimbo la Para, ambako mji wa Belem uliopo, ameambia vyombo vya habari vya nchini Brazil kwamba timu za dharura kwa sasa zinachunguza sababu mbili zinazowezekana za tukio hilo -- hitilafu ya jenereta au mzungumko mfupi wa umeme katika moja ya mabanda yaliyojengwa kwa ajili ya mkutano huo.

Wafanyakazi wa usalama wakiunda mnyororo wa binadamu kuongoza watu wanaokimbia kujiokoa kwenye eneo la Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP30) baada ya moto kuzuka mjini Belem, Jimbo la Para, Brazil, Novemba 20, 2025. (Picha na Lucio Tavora/Xinhua)

Askari wa zimamoto na wafanyakazi wakikagua eneo la Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP30) baada ya moto kuzuka mjini Belem, Jimbo la Para, Brazil, Novemba 20, 2025. (Picha na Lucio Tavora/Xinhua)

Watu wakikimbia kujiokoa kwenye eneo la Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP30) baada ya moto kuzuka mjini Belem, Jimbo la Para, Brazil, Novemba 20, 2025. (Picha na Lucio Tavora/Xinhua)

Wafanyakazi wa usalama wakiondoa watu ili kuwaokoa ndani ya eneo la Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP30) baada ya moto kuzuka mjini Belem, Jimbo la Para, Brazil, Novemba 20, 2025. (Picha na Lucio Tavora/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha