Lugha Nyingine
Ukarabati wa nyumba zaidi ya 32,500 wakamilika baada ya tetemeko la ardhi mkoani Xizang, China
Picha iliyopigwa Novemba 12, 2025 ikionyesha nyumba zilizojengwa upya ambazo zimekabidhiwa kwa wakazi katika Kijiji cha Yejiang cha Wilaya ya Dingri, Mji wa Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Jiang Fan)
XIGAZE - Mwanzoni mwa mwezi Januari, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 lilitokea katika Wilaya ya Dingri ya Mji wa Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China na kusababisha maelfu ya nyumba kubomoka.
Miezi kumi baada ya kutokea tetemeko hilo la ardhi, nyumba zaidi ya 32,500 zilizoharibiwa au kubomolewa zimekarabatiwa au kujengwa upya na kukabidhiwa kwa wakazi walioathiriwa, mamlaka ya mji huo wa Xigaze imesema.
Katika muda usiozidi siku tatu baada ya tetemeko hilo la ardhi kutokea, mkoa huo wa Xizang ulianzisha mpango wa ujenzi upya wa baada ya maafa na kuanza kazi ya kipindi cha kwanza cha kusafisha vifusi, kufanya utafiti na upimaji kwenye maeneo husika yaliyokumbwa na maafa, ili kufanya usanifu wa nyumba mpya.
Kazi hiyo ya ukarabati na ujenzi upya ilihusisha vijiji 486 katika wilaya saba, kujenga upya nyumba zaidi ya 22,000 na kukarabati nyumba nyingine 10,500 zisizopata uharibifu mbaya. Kundi la kwanza la wakazi walioathiriwa na tetemeko hilo la ardhi walihamia kwenye nyumba mpya mwezi Agosti mwaka huu.
Mwanakijiji mzee akiwa ameketi kwenye nyumba yake mpya katika Kijiji cha Qaba cha Wilaya ya Dingri, Mji wa Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Novemba 13, 2025. (Xinhua/Jiang Fan)
Mwanakijiji akichora picha ya ukutani iliyo ya mapambo ya ndani ya nyumba katika Kijiji cha Duoma cha Wilaya ya Lnaze ya Mji wa Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Novemba 20, 2025. (Xinhua/Ding Hongfa)
Picha hii iliyopigwa Novemba 13, 2025 ikionyesha nyumba zilizojengwa upya (zile zilizo kwenye ardhi ya juu) ambazo zimekabidhiwa kwa wakazi katika Kijiji cha Chagnag cha Wilaya ya Dingri ya Mji wa Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Jiang Fan)
Picha hii iliyopigwa Novemba 20, 2025 ikionyesha wanakijiji wakiwa kwenye nyumba yao katika Kijiji cha Duoma cha Wilaya ya Lnaze ya Mji wa Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Ding Hongfa)
Wanakijiji wakipiga picha ya familia mbele ya nyumba yao mpya kwenye Kijiji cha Cuoang cha Tarafa ya Qulho katika Wilaya ya Dingri ya Mji wa Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Oktoba 27, 2025. (Picha na Chen Xiaojun/Xinhua)
Mwanakijiji (wa pili, kushoto) akiwa amekaribisha majirani kwenye nyumba yake mpya katika Kijiji cha Gyabug cha Wilaya ya Dingri ya Mji wa Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Oktoba 24, 2025. (Xinhua/Jiang Fan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



