Lugha Nyingine
Wakimbizi karibu 12,000 wa Afghanistan warudi nyumbani ndani ya siku moja

Mtoto akionekana kutoka kwenye hema la msaada uliotolewa na China mjini Kabul, Afghanistan, Novemba 23, 2025. (Picha na Saifurahman Safi/Xinhua)
KABUL – Ofisi ya Kamishena waandamizi ya Afghanistan ya Kushughulikia Matatizo ya Watu Wanaorudi Nyumbani imesema jana Jumapili kwamba jumla ya familia 2,102 za Afghanistan zenye watu 11,855 zimerejea katika nchi yao kutoka nchi jirani za Iran na Pakistan juzi Jumamosi.
Ofisi hiyo imetoa huduma za kuwapatia wakimbizi hao waliorudi nyumbani makazi ya muda, lishe, maji, matibabu, na usafiri.
Hivi sasa wakimbizi karibu milioni sita wa Afghanistan, ambao wengi wao ni wahamiaji wasio na nyaraka halali, wanaishi nje ya nchi, na wengi kati yao wakiishi Iran na Pakistan.

Mtoto akionekana kwenye kambi ya muda mjini Kabul, Afghanistan, Novemba 23, 2025. (Picha na Saifurahman Safi/Xinhua)

Wakimbizi wa Afghanstan waliowasili punde wakipokea maji kwenye kambi ya muda mjini Kabul, Afghanistan, Novemba 23, 2025. (Picha na Saifurahman Safi/Xinhua)

Mtoto aliyewasili punde akinywa maji kwenye kambi ya muda mjini Kabul, Afghanistan, Novemba 23, 2025. (Picha na Saifurahman Safi/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



