Rais Xi asema China na Marekani zinapaswa kudumisha hali ya uhusiano, kusonga mbele kwa kufuata mwelekeo sahihi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu alipokuwa akizungumza na Rais wa Marekani Donald Trump kwa njia ya simu amesema kwamba China na Marekani zinapaswa kudumisha hali ya uhusiano, na kuendelea kusonga mbele kwa kufuata mwelekeo sahihi kwenye msingi wa kuwa na usawa, kuheshimiana na kunufaishana.

Rais Xi amesema kuwa yeye na Trump walifanya mkutano wenye mafanikio huko Busan mwezi uliopita, na kufikia maoni mengi muhimu ya pamoja.

"Yalirekebisha kwa usahihi mwelekeo wa meli kubwa ya uhusiano kati ya China na Marekani na kutoa msukumo zaidi kwake kusonga mbele kwa kasi tulivu, na hivyo kutoa ishara ya kuhimiza juhudi kwa dunia," amesema, akiongeza kuwa tangu wakati huo, uhusiano kati ya China na Marekani kwa ujumla umedumisha hali tulivu na kuhimiza juhudi, hali ambayo imekaribishwa na nchi hizo mbili na jumuiya pana ya kimataifa.

Amesema kile kilichotokea kinadhihirisha kwa mara nyingine tena kwamba maana ya ushirikiano kati ya China na Marekani kunufaisha pande zote mbili na mapambano kuumiza pande zote mbili inaonyesha mantiki ya kawaida ambayo imekuwa ikithibitishwa mara kwa mara katika uzoefu, na matarajio ya China na Marekani ya kusaidiana na kustawi kwa pamoja ni mustakabali halisi unaoweza kufikiwa.

Amesema pande hizo mbili zinapaswa kuongeza orodha ya mambo ya ushirikiano na kufupisha orodha ya matatizo, ili kupata maendeleo mengi ya kuhimiza juhudi, kujenga nafasi mpya ya ushirikiano kati ya China na Marekani na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi zote mbili na dunia.

Rais Xi ameelezea msimamo wa kikanuni wa China kuhusu suala la Taiwan, akisisitiza kwamba Taiwan kurudi kwa China ni sehemu muhimu ya utaratibu wa kimataifa wa baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Huku akisisitiza kwamba China na Marekani zilishirikiana bega kwa bega katika kupambana na ufashisti na matumizi ya nguvu za kijeshi, na hivi sasa pande hizo mbili zinatakiwa zaidi kulinda kwa pamoja ushindi wa Vita vya Pili vya Dunia (WWII).

Kwa upande wake Rais Trump amesema kuwa Rais Xi ni kiongozi mzuri, alifurahia sana mkutano wake na Rais Xi huko Busan, na anakubaliana na maoni yote aliyoyatoa Rais Xi kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa pande hizo mbili zinatekeleza mambo yote ya maoni ya pamoja waliyofikia viongozi hao wawili huko Busan.

“China ilikuwa imeonesha umuhimu wake katika ushindi wa Vita vya Pili vya Dunia,” amesema Trump, akisisitiza kwamba Marekani inaelewa umuhimu wa suala la Taiwan kwa China.

Marais hao wawili pia wamejadili msukosuko wa Ukraine. Rais Xi amesisitiza uungaji mkono wa China kwa juhudi zote ambazo ni mwafaka kwa amani, na kuelezea matumaini kwamba pande mbalimbali zitapunguza migongano kati yao, kufikia mapema iwezekanavyo makubaliano ya amani yenye usawa, ya kudumu na yenye nguvu ya kujizuia, na kupata ufumbuzi wa msukosuko huo kutokea katika chanzo chake. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha