Wilaya ya Baisha mkoani Hainan, China yaendeleza Mnyororo wa Tasnia ya Ruba ya Matibabu ili Kuhimiza Maendeleo yenye Sifa Bora ya Uchumi wa Afya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2025

Tasnia ya hirudo, au ruba wa matibabu katika Wilaya ya Baisha, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China inawakilisha sekta ya kipekee ndani ya mnyororo wa viwanda wa uchumi wa afya.

Hirudo, ana vitu vingi vinavyofaa kwa mambo mbalimbali kama vile hirudin na hupatikana zaidi katika mikoa mitano ya kusini mwa China ukiwemo mkoa wa Hainan.

Kwa mujibu wa Xu Shihong, Mkurugenzi wa Kamisheni ya Afya ya Wilaya Inayojiendesha ya Kabila la Wali ya Baisha katika mkoa huo, mwezi Agosti 2024, wilaya hiyo ya Baisha ilizindua 'Utafiti wa Ufanisi wa Dawa za Hirudo za Hainan na Mradi wa Kufungamanisha Tasnia-Taaluma-Utafiti- Matibabu'.

Mpango huo ulianzisha kituo cha kwanza maalum cha kilimo cha kimatibabu cha ruba mwenye ncha ya dhahabu wa Hainan (Hirudo medicinalis) na kliniki mahsusi ya wagonjwa wasiohitaji kulazwa iliyobobea katika matumizi yake ya nje ya mwili.

Kwa sasa, kituo sanifu cha kuzaliana na kufuga ruba wa matibabu hutoa zaidi ya 100,000 kwa mwaka. Kliniki maalum inayotoa tiba ya nje ya mwili kwa ruba hao pamoja na vipande vya ruba vilivyokaushwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya mwili imeanza kufanya kazi rasmi katika Tawi la Baisha la Hospitali ya Mkoa wa Hainan.

Kimsingi inatibu hali zikiwemo za carotid artery plaque, spondylosis ya shingo, madhara baada ya kiharusi, shinikizo la juu la damu, hyperlipidemia, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine ya moyo na mishipa ya damu, pamoja na rheumatic (rheumatoid) arthritis, gout na matatizo mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa usawa wa yin-yang mwilini na kuzuiwa kwa qi pamoja na stasis ya damu.

Mkurugenzi Xu Shihong wa tiba hiyo ameelezea mpango wa kuanzisha mnyororo kamili wa viwanda wa Hirudo nipponica maalum kwa wilaya ya Baisha, unaojumuisha:

Kwanza, kuanzisha mnyororo kamili wa viwanda wa 'ufugaji-uzalishaji-mauzo-huduma'. Kwa kuanzia kwenye misingi iliyopo ya ufugaji, amesema wataboresha zaidi mbinu za ufugaji, mbinu za usindikaji, kusanifisha matumizi ya kimatibabu, na kukuza chapa ya kwenye soko ili kuikuza tasnia ya ruba kuwa sekta ya kipekee na yenye faida kwa Wilaya ya Baisha.

Pili, kuharakisha maendeleo ya 'Mradi wa Kielelezo wa Tasnia, Taaluma na Utafiti wa Ruba wa Hainan'. Amesema hiyo inahusisha kuhimiza kwa nguvu zote mipango kama vile 'tiba ya nje ya mwili kwa ruba' na ufugaji wa ruba wa matibabu wasio na vimelea vya magonjwa.’ Amesema, watahimiza mfumo wa 'kampuni + wafugaji' huku wakati huohuo wakiendeleza viwanda vya usindikaji wa kina wa ruba, kuendeleza utengenezaji wa vipande vya mitishamba na uzalishaji wa dawa ili kupanua mnyororo wa viwanda na kuboresha thamani za nyongeza.

Tatu, amesema wataanzisha chapa ya mkoa ya 'Ruba wa Hainan' ili kuongeza uelewa kuhusu thamani ya kimatibabu ya ruba na sifa zake za kipekee.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha