Ziwa Qionghai la China ambalo lilikuwa limechafuliwa lashuhudia kuongezeka kwa spishi za ndege baada ya ikolojia kuboreshwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2025

Ndege wa Glossy Ibisi wakionekana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Qionghai katika Mji wa Xichang, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Novemba 11, 2025. (Xinhua)

Ndege wa Glossy Ibisi wakionekana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Qionghai katika Mji wa Xichang, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Novemba 11, 2025. (Xinhua)

CHENGDU - Idadi ya spishi za ndege kwenye Ziwa Qionghai katika Mji wa Xichang, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China imefikia 310 mwaka huu, idadi ambayo ni ya juu zaidi katika historia. Na idadi kubwa zaidi ya ndege wanaohamahama imekuwa wakazi wa kudumu kutokana na kuboreshwa kwa hali ya ikolojia, mamlaka za serikali za mitaa zimesema Jumapili.

Kituo cha uhifadhi cha Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Qionghai kimesema ongezeko hilo limetokana na kuimarishwa kwa urejeshaji wa mazingira na kupungua kwa shughuli za binadamu. Yang Jun, mhandisi mwandamizi wa idara ya misitu na mbuga ya Xichang, amesema kwamba spishi saba za ndege wanaohamahama, zikiwemo Eurasia coot, white-breasted waterhen na Asian openbill, sasa zimeishi hapa kama wakazi.

Takwimu za ufuatiliaji zinaonyesha kuwa ziwa hilo lilikuwa na spishi 120 za ndege mwaka 2014, huku idadi ikiongezeka hadi 302 ilipofika mwaka 2024, na sasa imefikia 310. Miongoni mwa spishi hizo, tano ni ndege walio katika ulinzi wa daraja la kwanza kitaifa na 47 ni walio katika ulinzi wa daraja la pili, zikiwemo spishi adimu kama vile purple swamphen na Chinese merganser, ambazo zinakua vizuri katika ziwa hilo.

Ziwa Qionghai, ziwa la pili kwa ukubwa la ndani ya bara la Sichuan, lilikabiliwa na uharibifu mkubwa kuanzia miaka ya 1960 hadi 1990 kutokana na kutwaa eneo la ziwa kwa ajili ya kilimo, eneo la maji yake lilipungua na idadi ya spishi za ndege ilishuka hadi zaidi ya 20 tu.

Kutokana na juhudi za miaka ya hivi karibuni, kama vile miradi ya kurejesha maeneo ya kando ya ziwa, kuhamisha wakazi zaidi ya 50,000 na kujenga mu 20,000 (hekta karibu 1,333) za ardhi oevu, zaidi ya kilomita 30 za pwani ya asilia zimerudishwa.

Watazamaji wa ndege wamegundua kuwa makazi ya ndege yalipanuka na spishi za ndege katika eneo hilo zimeongezeka, na Qionghai sasa imeorodheshwa kuwa miongoni mwa maeneo bora ya kutazama ndege mkoani Sichuan. China ni ushoroba muhimu wa uhamaji wa ndege, ambayo ina njia nne kati ya tisa kuu za kuhama kwa ndege wanaohamahama duniani. Imeanzisha maeneo ya ardhi oevu zaidi ya 2,200 yanayolindwa na maeneo 82 ya ardhi oevu muhimu kimataifa -- ikidumisha ukubwa wa eneo la ardhi oevu huku kukiwa na ahadi za kimataifa za mazingira. 

Ndege akiruka juu ya maji kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Qionghai katika Mji wa Xichang, Mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China, Novemba 17, 2025. (Xinhua)

Ndege akiruka juu ya maji kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Qionghai katika Mji wa Xichang, Mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China, Novemba 17, 2025. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha