Benki ya Dunia yainua makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Kenya mwaka huu hadi asilimia 4.9

(CRI Online) Novemba 25, 2025

Benki ya Dunia imeinua makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa mwaka huu hadi kufikia asilimia 4.9, likiwa ni ongezeko kutoka asilimia 4.5 ya mwezi Mei, ikirejelea ni kuimarika kwa kasi kuliko ilivyotarajiwa katika sekta ya ujenzi.

Ripoti ya Uchumi wa Kenya iliyotolewa na benki hiyo mjini Nairobi, imesema kuwa mfumuko wa bei wa chini, sera za fedha za kutuliza uchumi, kuboreshwa kwa utoaji wa mikopo kutokana na mazingira mazuri ya kifedha, vinatarajiwa kuunga mkono kuongeza mapato ya kaya na uwekezaji binafsi.

Kwa mujibu wa benki hiyo, makadirio hayo ya ukuaji wa muda wa kati yanatarajiwa kuunga mkono ongezeko la mapato halisi kwa kila mtu, lakini kiwango cha kupunguza umaskini kitaendelea kuwa cha chini, isipokuwa kama ukuaji huo utasaidia kuongeza mapato na kuleta ajira bora, hasa kwa watu maskini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha