Lugha Nyingine
Rais Xi ahimiza mikoa yenye uchumi mkubwa kuongeza maarifa ya kutatua matatizo mapya

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 5, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ameihimiza mikoa ya China yenye uchumi mkubwa zaidi kufanya juhudi maradufu ili kuongeza maarifa katika kuchambua hali mpya na kutatua matatizo mapya.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo jana Alhamisi wakati akishiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China.
"Ili kutimiza malengo ya maendeleo ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030), China lazima ikabiliane na mazingira magumu zaidi na kutatua migongano kwenye ngazi ya kina zaidi ," amesema.
Baada ya kusikiliza hotuba za wajumbe wa Bunge la Umma, Rais Xi ametoa matakwa kwa mkoa wa Jiangsu wa mashariki mwa China wenye nguvu zaidi kiuchumi katika kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na jamii ya miaka mitano ijayo.
Amesema baada ya kuwa na msingi imara mkoa huo unapaswa kuongoza maendeleo ya nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora, kazi hii ni muhimu zaidi katika kusukuma mbele maendeleo yenye sifa bora na kuongeza nguvu ya kufanya ushindani wa kiuchumi.
Rais Xi ameuhimiza mkoa huo kuhimiza maendeleo ya utandawazi wa elimu, teknolojia na vipaji, na kujitahidi kupata mafanikio mapya katika uvumbuzi halisi na teknolojia za msingi katika sekta muhimu.
"Mkoa wa Jiangsu unapaswa kuanzisha hali mpya katika kuboresha viwanda vya kijadi, kuandaa viwanda vinavyoibukia, na kupanga mipango ya viwanda vya kutupia macho siku za baadaye," Rais Xi amesema, akitoa wito wa kujipatia maendeleo mapya katika kuendeleza kwa kina mageuzi na kuondoa vizuizi vya kimfumo kwa maendeleo ya nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.
Rais Xi akisisitiza kazi muhimu za nguzo za mikoa yenye uchumi mkubwa katika kuimarisha utulivu wa uchumi wa nchi, amesema kwamba mkoa wa Jiangsu unatakiwa kuendelea kuimarisha uhimilivu wake wa kiuchumi na kujifungamanisha kwa kina kwenye soko la pamoja la nchini, huku ukipanua ufunguaji mlango kwa vigezo vya juu na kupanua ufikiaji wake kwenye masoko duniani.
Cai Qi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, alishiriki kwenye majadiliano hayo.

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu katika mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Picha na Sheng Jiapeng/Xinhua)

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu katika mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu katika mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma