Viongozi wa China wahudhuria vikao vya majadiliano kwenye mkutano wa mwaka wa bunge

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2026

Li Qiang, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China, akijumuika na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Yunnan kuchunguza ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 5, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

Li Qiang, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China, akijumuika na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Yunnan kujadili ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 5, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Viongozi waandamizi wa China jana Alhamisi walihudhuria vikao vya majadiliano kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), bunge la kitaifa la China.

Alipojumuika na wajumbe wa bunge kutoka Mkoa wa Yunnan katika mjadala wa kundi, Waziri Mkuu Li Qiang amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa kwanza wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) huku kukiwa na kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika katika mazingira ya nje na kazi ngumu katika mageuzi na maendeleo ya ndani.

Li amehimiza kuchukua hatua chanya zaidi za mapema na za kivitendo ili kukabiliana vyema na hatari na changamoto mbalimbali.

Spika wa Bunge la China Zhao Leji alishiriki kwenye majadiliano ya pamoja na wajumbe kutoka Mkoa wa Sichuan, akihimiza utekelezaji thabiti na wa kina wa kazi zote ili kuwa na mwanzo mzuri wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano.

Mwenyekiti wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) Wang Huning alijumuika na wajumbe wenzake kutoka Mkoa wa Guizhou katika majadiliano ya pamoja, akitoa wito kwa mkoa huo kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora kulingana na hali za mkoa huo, na kuhimiza mafungamano ya kina ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na uvumbuzi wa viwanda.

Naibu Waziri Mkuu Ding Xuexiang, alipojumuika kwa majadiliano na wajumbe wenzake kutoka Mkoa wa Liaoning, amesisitiza kufuata ukuaji halisi badala ya usio halisi, na kuhimiza maendeleo yenye sifa bora na endelevu.

Li Xi, katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC alijumuika na wajumbe wenzake kutoka Mkoa wa Fujian katika majadiliano ya pamoja. Amewahimiza wanachama na maofisa wa Chama kudumisha mtazamo sahihi kuhusu ufanisi wa utawala.

Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Ding Xuexiang, na Li Xi wote ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.

Alipokuwa akizungumza na wajumbe kutoka Mkoa wa Shandong, Makamu wa Rais Han Zheng amehimiza juhudi za kuhakikisha mwanzo mzuri wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano.

Zhao Leji, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama ambaye pia ni spika wa Bunge la Umma la China, akishiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Sichuan kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

Zhao Leji, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama ambaye pia ni spika wa Bunge la Umma la China, akishiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka ujumbe wa Mkoa wa Sichuan kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

Wang Huning, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) akishiriki kwenye kikao cha majadiliano na wajumbe wa mkoa wa Guizhou kuchunguza ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China, mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Wang Huning, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) akishiriki kwenye kikao cha majadiliano na wajumbe wa mkoa wa Guizhou kujadili ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China, mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Ding Xuexiang, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Naibu Waziri Mkuu wa China akijmuika na wajumbe wa mkoa wa Liaoning kuchunguza ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China, mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

Ding Xuexiang, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Naibu Waziri Mkuu wa China akijmuika na wajumbe wa mkoa wa Liaoning kujadili ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China, mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

Li Xi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC,  akijumuika na wajumbe wa mkoa wa Fujian kuchunguza ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China, mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)

Li Xi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, akijumuika na wajumbe wa mkoa wa Fujian kujadili ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China, mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)

Makamu wa Rais Han Zheng akijumuika na wajumbe wenzake wa mkoa wa Shandong kuchunguza ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China, mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)

Makamu wa Rais Han Zheng akijumuika na wajumbe wenzake wa mkoa wa Shandong kujadili ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China, mjini Beijing, China, Machi 5, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha