Lugha Nyingine
Bunge la Umma la China lapitia muswada wa sheria wa mpango wa maendeleo ya nchi
BEIJING - Bunge la Umma la China jana Alhamisi lilianza kujadili muswada wa sheria ambao unaweka kanuni za kutungwa na kutekelezwa kwa mpango wa maendeleo ya nchi wa miaka mitano.
Muswada huo wa sheria wa mpango wa maendeleo ya nchi uliwasilishwa kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge la Umma la China kwa kujadiliwa na kupitishwa.
Kazi hii ya kupitia mswada huo ilifanyika katika wakati wa wajumbe wa bunge hilo kuthibitisha mswada wa mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa nchi, ambao utaelekeza maendeleo ya nchi ya China, uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, kuanzia mwaka 2026 hadi 2030.
Waraka wa maelezo uliowasilishwa kwenye mkutano wa bunge la umma la China unaeleza kuwa, muswada huo wa sheria umetokana na maarifa muhimu ya muda mrefu wa China katika utungaji wa mipango ya maendeleo ya nchi, ukiweka kanuni za kivitendo zenye ufanisi mzuri kwenye mfumo wa sheria kwa kulenga kuimarisha kazi ya uelekezaji wa kimkakati kwa utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya nchi.
Muswada huo wa sheria uliogawanywa katika sura sita, unaweka vifungu kuhusu kutungwa, kuthibitishwa, kupitishwa, kutekelezwa, pamoja na kufanya usimamizi kwa utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya nchi.
Tokea mwaka 1953, China imeunda na kutekeleza mipango 14 ya miaka mitano, mipango hiyo ambayo inasaidia kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na jamii, kuboresha kiwango cha maisha, na kuimarisha nguvu zote za nchi nzima.
Muswada wa sheria hiyo unarasmisha mchakato ambao Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kutoa mapendekezo, Baraza la Serikali la China kuandaa mpango, na Bunge la Umma la China kuthibitisha na kuidhinisha mpango, hatimaye kutolewa kwa mpango.
Muswada huo umedhihirisha kuwa, mipango ya maendeleo ya nchi inapaswa kuelezea bayana nia za kimkakati za China na kazi muhimu ya serikali, na kuelekeza mashirika mbalimbali ya jamii kuanzisha shughuli husika.
Muswada wa sheria hiyo pia unasisitiza umuhimu wa kusikiliza maoni na mashauri ya umma katika mchakato wa kupangwa kwa mpango. Katika mwaka uliopita, mamlaka husika ilianzisha shughuli ya kusikiliza maoni na mashauri ya umma mtandaoni kwa mwezi mmoja kuhusu Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, na kupata majibu zaidi ya milioni 3.11. Maofisa wamesema kuwa maoni hayo yamechangia utungaji wa mpango huo.
Waraka wa maelezo ya mswada huo umesema kuwa, kutolewa kwa sheria hiyo ni hatua muhimu ya demokrasia ya umma ya mchakato mzima wa kutekeleza mpango wa maendeleo ya nchi.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma