China yatoa wito wa kupinga kithabiti mapambano dhidi ya ugaidi yanayochagua na ya vigezo viwili

(CRI Online) Machi 06, 2026

Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong amesema, jumuiya ya kimataifa lazima ipinge kithabiti mapambano dhidi ya ugaidi yanayochagua na ya vigezo viwili, na kutokomeza vyanzo vya ugaidi kwa kupunguza migogoro, umaskini, na kuheshimu uanuwai wa ustaarabu.

Akizungumza Jumatano wiki hii kwenye kikao cha kupewa taarifa juu ya "Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ugaidi Duniani", Balozi Fu amesema mkakati huo tangu upitishwe miaka 20 iliyopita, umechangia katika kuzuia na kupambana na ugaidi, kuimarisha ujengaji uwezo wa nchi wanachama katika kupambana na ugaidi, na kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika nyanja hiyo.

Amesema China inaunga mkono Umoja wa Mataifa kuendelea na jukumu lake muhimu la kufanya uratibu.

Balozi Fu pia amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika na Umoja wa Afrika na kuiunga mkono Afrika kuimarisha uwezo wake katika kupambana na ugaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha