Lugha Nyingine
Iran yasema haijaomba kusimamisha vita na inajiandaa kwa uvamizi wa ardhini kutoka Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi kwenye mahojiano na Shirika la Habari la Marekani, ABC jana Alhamisi amesema kuwa licha ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi ya anga kote Iran, nchi hiyo haijaomba kusimamisha vita, na inajiandaa kwa uvamizi wa ardhini kutoka Marekani.
Amesema kwamba Marekani iliishambulia Iran wakati wa mazungumzo mwaka jana na mwaka huu, kwa hiyo Iran haina sababu ya kuwasiliana na "wanaokosa udhati kwenye mazungumzo na wasioshiriki kwenye majadiliano kwa nia njema."
Kuhusu uwezekano wa mashambulizi hayo ya ardhini ya Marekani, Araqchi amesema "tunayasubiria kwa sababu tunajiamini katika kuyakabili na hilo litakuwa balaa kubwa kwao.”

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma