Lugha Nyingine
Majimbo zaidi ya 20 ya Marekani kuzuia mpango mpya wa ushuru wa Trump
Jimbo la Oregon, kwa pamoja na majimbo mengine 23 ya Marekani yamefungua kesi mahakamani jana Alhamisi yakitafuta kuzuia duru mpya ya ushuru iliyotangazwa na Rais wa Marekani, Donald Trump.
Kesi hiyo, iliyowasilishwa katika Mahakama ya Biashara ya Kimataifa ya Marekani, inasema kwamba sera hiyo ya ushuru inakiuka sheria ya serikali kuu, inadhoofisha mgawanyo wa madaraka kikatiba, na inakiuka Sheria ya Utaratibu wa Utawala.
Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la Oregon Dan Rayfield amesema katika taarifa kwamba, kesi hiyo inalenga kupinga mpango huo wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kutoza ushuru wa ziada wa 15% kwa sehemu nyingi za dunia bila idhini kutoka Bunge la Marekani, Congress.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo hiyo, Rais Trump aliweka ushuru kwa zaidi ya mwaka mmoja bila mamlaka halali ya kisheria.
Hata hivyo, tarehe 20 Februari mwaka huu, Mahakama Kuu ya Marekani ilitoa uamuzi kwamba, hatua za ushuru huo za serikali ya Rais Trump chini ya Sheria ya Dharura ya Kimataifa ya Mamlaka za Kiuchumi hazikuwa na idhini ya kisheria iliyo wazi. Trump ametumia sheria nyingine, Kifungu cha 122 cha Sheria ya Biashara ya 1974, na kutangaza ushuru mpya wa asilimia 15 kwa bidhaa nyingi duniani kote, akirejelea nakisi ya biashara kuwa ni sababu, taarifa hiyo imesema.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma