Lugha Nyingine
"Barabara ya sukari" iliyojengwa na Kampuni ya China yawezesha maendeleo ya magharibi mwa Kenya

Watoto wawili wa kiume wakiosha miwa kando ya eneo la ujenzi wa sehemu ya pili ya mradi wa barabara kuu ya Kisumu-Muhoroni inayojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Nishati ya China kwenye eneo kuu linalozalisha miwa la Kaunti ya Kisumu, Kenya, Februari 27, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)
KISUMU, Kenya - Akitazama malori mazito yaliyojaa miwa yakisafiri kwa urahisi kwenye barabara mpya ya lami kuelekea kiwanda cha mbali, mkulima Rosslyn Akini Abudo mwenye umri wa miaka 43 hawezi kuficha kuridhika kwake.
"Kabla, hakukuwa na barabara. Kusafirisha miwa kupitia mashamba yenye matope kwa kutumia punda na matrekta ilikuwa ni mateso tupu," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye mahojiano ya hivi karibuni.
Ikiwa ipo katika Kaunti ya Kisumu, kitovu muhimu cha kiuchumi na usafirishaji katika magharibi mwa Kenya, eneo hilo linajulikana sana kwa kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari. Mradi huo wa barabara unaotekelezwa na Kampuni ya Ujenzi wa Nishati ya China (PowerChina) sasa unaleta mabadiliko halisi katika eneo hilo.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 40 inayopitia maeneo makuu ya kilimo cha miwa katika kaunti hiyo, ikiunganisha mashamba makubwa na viwanda vya sukari vya eneo hilo na kuingiza msukumo mpya kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya kaunti hiyo.
Abudo amesema kwamba anamiliki ekari mbili za miwa, na "kuuza mavuno yote kunaweza kunipatia shilingi 100,000 (dola za Marekani takribani 773)."
Kwa mujibu wa Li Yingtao, meneja wa mradi wa PowerChina katika kaunti hiyo ya Kisumu, barabara hiyo inaunda sehemu ya pili ya mradi wa barabara kuu ya Kisumu-Muhoroni.
Wakazi wameipa jina la utani "Barabara ya Sukari," Li amesema, akisema kuwa inapitia katika ukanda mkuu wa miwa wa eneo hilo na ni njia muhimu ya usafirishaji kwa eneo la magharibi mwa Kenya.
Kwa sasa, asilimia karibu 35 ya mradi huo imekamilika, na kazi zote za mkataba zinatarajiwa kukamilika ndani ya miezi takriban 18.
Mara itakapokamilika, barabara hiyo itaunganisha ukanda wa sukari wa Kenya na kuungana na barabara kuu inayoelekea mpakani mwa Uganda, ikiboresha kwa kiasi kikubwa muunganisho wa kikanda.
Akisema kuwa kampuni hiyo inaweka umuhimu mkubwa kwenye shughuli za kienyeji, Li amesema kwamba wapimaji, wasanifu, madereva na waendeshaji vifaa katika eneo la ujenzi wote ni waajiriwa wenyeji, na mchakato wa ujenzi umetengeneza moja kwa moja ajira zaidi ya 200, ukileta manufaa halisi kwa wakulima wenyeji.
Hadi sasa, PowerChina imeshajenga barabara 31 za vijijini nchini Kenya, zenye jumla ya urefu wa kilomita zaidi ya 1,580. Kwa kuzingatia usimamizi wa wenyeji, miradi hiyo ya barabara imezalisha ajira nyingi kwa wenyeji na kuwapa mafunzo wafanyakazi wengi wa kiufundi.
David Maganda, mhandisi msimamizi wa serikali ya Kenya kwa mradi huo, amekuwa akifanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye eneo la ujenzi tangu ujenzi huo uanze.
Mhandisi huyo, ambaye amekuwa akishirikiana na PowerChina kwa miaka mingi, amesifu kazi za zamani za kampuni hiyo katika eneo hilo. "Miradi iliyopita ilikuwa bora, imekuwa miradi alama na ya kiwango cha mfano katika kaunti ya Kisumu," Maganda amesema.

Picha iliyopigwa tarehe 27 Februari, 2026 ikionyesha magari ya ujenzi na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Nishati ya China wakifanya kazi kwenye eneo la ujenzi wa sehemu ya pili ya mradi wa barabara kuu ya Kisumu-Muhoroni katika eneo kuu la uzalishaji a Kaunti ya Kisumu, Kenya. (Xinhua/Xie Jianfei)

Picha iliyopigwa tarehe 27 Februari, 2026 ikionyesha eneo la ujenzi wa sehemu ya pili ya mradi wa barabara kuu ya Kisumu-Muhoroni inayojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Nishati ya China katika eneo kuu la uzalishaji miwa la Kaunti ya Kisumu, Kenya. (Xinhua/Xie Jianfei)

Magari ya ujenzi na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Nishati ya China wakifanya kazi kwenye eneo la ujenzi wa sehemu ya pili ya mradi wa barabara kuu ya Kisumu-Muhoroni katika eneo kuu la uzalishaji miwa la Kaunti ya Kisumu, Kenya, Februari 27, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Picha iliyopigwa tarehe 27 Februari, 2026 ikionyesha eneo la ujenzi wa sehemu ya pili ya mradi wa barabara kuu ya Kisumu-Muhoroni inayojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Nishati ya China katika eneo kuu la uzalishaji miwa la Kaunti ya Kisumu, Kenya. (Xinhua/Xie Jianfei)

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma