Lugha Nyingine
Wataalamu wa afya wa China waboresha uelewa wa afya wa wanawake Tanzania Zanzibar
Timu ya wataalamu wa China inayosaidia mradi wa kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kichocho wa Zanzibar, Tanzania imefanya tukio la elimu ya afya jana Alhamis kuhusu ugonjwa huo katika via vya uzazi vya wanawake kwenye shule moja ya msingi kisiwani Pemba.
Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Vimelea ya Jiangsu, Li Wei amesema, tukio hilo lililofanyika kabla ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka, ilizingatia afya ya mabinti na jinsi ya kuzuia magonjwa shuleni, na ilivutia walimu na wanafunzi zaidi ya 400.
Amesema kichocho katika via vya uzazi vya mwanamke, ambayo ni dalili kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa kichocho, kinaweza kuwa na athari za muda mrefu kwa afya ya uzazi ya mwakamke kama hakitashughulikiwa mapema.
Ofisa wa afya kisiwani Pemba, Mohamed Nassor Salim amesema, tukio hilo linaonyesha ahadi ya muda mrefu ya China katika kuunga mkono maendeleo ya afya kwa vijana.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma