Rais Xi asisitiza kuongeza utiifu wa kisiasa wa jeshi na kusukuma mbele mambo ya kisasa ya ulinzi wa nchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 09, 2026

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihudhuria kikao cha wajumbe wote wa ujumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) mjini Beijing, Machi 7, 2026. (Xinhua/Li Gang)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza kutumia vya kutosha na kuongeza nguvu bora ya kipekee ya utiifu wa kisiasa wa jeshi, na ametoa wito wa kuwataka watu wote kufanya juhudi za pamoja kwa moyo mmoja za kusukuma mbele kwa hatua madhubuti ujenzi wa mambo ya kisasa ya ulinzi wa taifa na ya vikosi vya jeshi.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Jeshi ya China (CMC), ameyasema hayo katika wakati wa kuhudhuria kikao cha wajumbe wote wa ujumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) siku ya Jumamosi, mjini Beijing.

Wajumbe sita walitoa hotuba kwenye kikao hicho. Baada ya kusikiliza maoni yao, Rais Xi alitoa hotuba muhimu.

Rais Xi amesema, tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC mwaka 2012, Kamati Kuu ya Chama ilikuwa imeweka dhamira na kutoa nguvu kubwa kuliko hapo kabla ikiongoza vikosi vya jeshi kuongeza marekebisho ya kisiasa na kuhimiza kuongeza utiifu wa kisiasa jeshini na kupata matokeo dhahiri.

“Lazima kusiwe na nafasi katika jeshi kwa wale ambao si watiifu kwa Chama, wala nafasi yoyote kwa wafisadi,” Rais Xi ameonya, akiongeza kuwa mapambano dhidi ya ufisadi lazima yaendelee kupiga hatua mbele kithabiti.

Rais Xi amesema, katika mwanzo wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030), ni lazima kufanya juhudi za kuweka kanuni za kufanya usimamizi kwa makini, na kufuatilia kwa karibu maeneo muhimu ya mzunguko wa fedha, matumizi ya madaraka, na udhibiti wa ubora.

“Ni lazima kuimarisha kikamilifu uongozi wa Chama na ujenzi wa jeshi, na kuzifanya oganaizesheni za Chama katika ngazi zote kuwa na nguvu zaidi,” Rais Xi amesema, akisisitiza kubadilisha nguvu halisi ya uongozi wa Chama kuwa mwelekeo wa maendeleo.

Rais Xi amesema ni muhimu kuimarisha hali ya kuhakikisha maofisa na askari wanafuata mwongozo wa Chama, na kuhakikisha silaha na zana na vifaa vya kisasa vinawekwa mikononi mwa watu wanaowajibika kisiasa.

Rais Xi ametoa wito wa kuwaandaa kwa utaratibu askari wanaoshiriki kwenye operesheni za pamoja, kuandaa aina mpya za vikosi vya kupigana vita, kufanya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia wa kiwango cha juu, na usimamizi wa kimkakati wa kiwango cha juu.

Pia amesisitiza juhudi za kutukuza na kuenzi desturi nzuri za Chama na jeshi.

Zhang Shengmin, naibu mwenyekiti wa CMC, alihudhuria kwenye mkutano huo.

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Jeshi ya China (CMC), akihudhuria kikao cha wajumbe wote wa ujumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) mjini Beijing, Machi 7, 2026. (Xinhua/Li Gang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha