Toleo Fupi la Ripoti ya Kazi ya Serikali ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 09, 2026

Tarehe 5, Machi, Waziri Mkuu wa China Li Qiang alitoa Ripoti ya Kazi ya Serikali kwenye Mkutano wa Nne wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China. Maudhui muhimu ya ripoti hiyo ni kama yanayofuata:

I. Kukumbuka Kazi ya Serikali ya China ya Mwaka 2025

Pato la Taifa (GDP) limeongezeka kwa 5%.

Nafasi mpya za ajira mijini ziliongezeka kwa milioni 12.67.

Uzalishaji wa nafaka umefikia tani milioni 715.

Uzalishaji wa mwaka wa magari ya nishati mpya umezidi milioni 16.

Katika miaka 5 iliyopita,

Wastani wa Pato la Taifa (GDP) uliongezeka kwa 5.4% kila mwaka

Thamani ya nyongeza ya viwanda vya utengenezaji bidhaa imeendelea kushika nafasi ya kwanza duniani kwa miaka 16 mfululizo.

Wastani wa mapato ya kila mkazi yanayoweza kutumika umeongezeka kwa 5.4% kila mwaka.

Nafasi mpya za ajira mijini kwa jumla zimeongezwa kwa zaidi ya milioni 60.

II. Malengo makuu na Majukumu Muhimu ya Kipindi cha "Mpango wa 15 wa Miaka Mitano"

Thamani ya jumla ya uzalishaji nchini yadumisha ongezeko la kufaa

Wastani wa ongezeko la mwaka la uwekezaji wa jumla katika Utafiti na Maendeleo (R&D) kwenye jamii nzima kuongezeka kwa zaidi ya 7%.

Kupunguza utoaji wa jumla wa kaboni (CO2) kwa kila thamani ya GDP kwa 17%.

Thamani ya nyongeza ya uzalishaji wa viwanda vikuu vya uchumi wa kidijitali itachukua 12.5% ya GDP nchini.

Wastani wa miaka ya kupata elimu kwa kila mtu aliyefikia umri wa kufanya kazi utaongezwa kuwa miaka 11.7.

Wastani wa miaka ya kuishi kwa kila mtu unakadiriwa kuongezwa hadi miaka 80.

Uwezo wa jumla wa uzalishaji wa nafaka utafikia tani milioni 725.

Uwezo wa jumla wa uzalishaji wa nishati kufikia tani bilioni 5.8 za makaa ya mawe ya kawaida.

III. Matakwa ya Jumla na Mwelekeo wa Sera kwa Maendeleo ya Uchumi na Jamii mwaka 2026

Ongezeko la uchumi: 4.5%~ 5%

Ongezeko la nafasi mpya za ajira mijini: Zaidi ya watu milioni 12.

Kiasi cha kupandishwa kwa Bei za vitu vya matumizi ya wakazi (CPI): Takriban 2%.

Uzalishaji wa nafaka : Tani milioni 700 hivi.

Utoaji wa CO2 kwa kila thamani ya GDP: Kupungua kwa 3.8% hivi.

Nakisi ya bajeti yanapangiwa kwa 4% hivi, na ukubwa wa nakisi utaongezeka kwa Yuan bilioni 230 kuliko mwaka uliopita.

Matumizi ya bajeti ya mambo ya umma: Yatafikia Yuan trilioni 30 kwa mara ya kwanza.

Dhamana maalum za kitaifa za muda mrefu zaidi : Yuan trilioni 1.3.

Dhamana maalum za serikali za mitaa: Yuan trilioni 4.4.

IV. Sehemu ya Majukumu ya Mwaka 2026

Kuongeza Mapato: Kutunga na kutekeleza mpango wa kuongeza mapato ya wakazi wa mijini na vijijini, na kuchukua hatua mbalimbali za kufuata hali halisi katika kuhimiza kazi ya kuwasaidia watu wenye mapato ya chini kuongeza mapato yao, kuongeza matapo ya kimali ya wakazi, na kukamilisha mifumo ya mishahara na huduma za jamii.

Matumizi: Kupangia dhamana maalum za kitaifa za Yuan bilioni 250 kwa kuunga mkono wakazi kubadilisha vyombo vya zamani vya matumizi nyumbani kuwa vyombo vipya.

Uwekezaji: Kutarajia kupangia uwekezaji wa Yuan bilioni 755 kutoka bajeti ya serikali kuu, na kupangia dhamana maalumu za kitaifa za muda mrefu za Yuan bilioni 800 kwa utekelezaji wa mikakati mikuu ya nchi na ujenzi wa uwezo wa usalama wa sekta muhimu.

Nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora: Kujenga viwanda nguzo vinavyoibuka kama vile saketi jumuishi (IC), usafiri kwenye anga na anga ya juu, matibabu na dawa za kibiolojia, na uchumi wa anga ya chini. Kuendeleza viwanda vya siku za baadaye kama vile vya nishati za baadaye, teknolojia ya quantum, roboti za AI , mfumo wa kuunganisha ubongo na kompyuta, na teknolojia ya 6G. Kuendeleza kwa kina “AI+”.

Soko kuu la pamoja la nchi nzima : kushughulikia kwa kina ushindani usioweza kuleta maendeleo kwa kupitia marekebisho na udhibiti wa uwezo wa uzalishaji, kuongoza uzalishaji kwa vigezo, kusimamia na kutekeleza sheria juu ya bei za vitu sokoni, na kusimamia ubora wa bidhaa.

Ufunguaji Mlango: Kupanua zaidi miradi ya majaribio katika sekta za huduma za mawasiliano ya habari, teknolojia za kiviumbe, na hospitali zilizoanzishwa na kuendeshwa na wawekezaji wa nchi za nje.

Ustawishaji wa pande zote wa Vijiji: Kuanzisha raundi ya pili ya majaribio ya mkoa mzima ya kuongeza tena muda wa miaka 30 kwa haki ya familia za wakulima zilizosaini mikataba za kuendesha na kusimamia ardhi za ushirika au za nchi. Kufanya sensa ya nne ya kilimo ya nchi nzima.

Maendeleo ya miji ya aina mpya: Kusukuma mbele kwa utaratibu na kwa njia ya kisayansi kazi ya kuwahesabu wakulima waliohamia mijini kuwa wa idadi ya wakazi mijini, na kurahisisha masharti ya kuandikisha katika sekondari kwa watoto wao kwa kufuata hali halisi ya kila sehemu.

Ajira: Kujenga njia ya kutoa kwanza nafasi za ajira katika mchakato wa maendeleo ya uchumi. Kuchukua hatua za kuimarisha nafasi za ajira, na kupanua nafasi bora za ajira.

Elimu: Kukamilisha sera ya elimu ya chekechea bila malipo, na kuongeza utoaji wa shahada ya sekondari ya kawaida.

Matibabu na Afya: kuongeza Yuan 24 za ruzuku ya bima ya afya kwa kila mkazi.

Uhakikisho wa Kijamii: Kuongeza tena Yuan 20 kwa kiwango cha chini zaidi cha ruzuku ya utunzaji wa uzeeni ya kila mwezi. Kuimarisha uhakikisho wa nyumba za kuishi kwa watu waliooana kwa mara ya kwanza na wazazi waliozaa mtoto kwa mara ya kwanza, na kuunga mkono mahitaji ya kuboresha nyumba za kuishi kwa kila familia yenye watoto zaidi ya mmoja.

Maendeleo ya Kijani: Kuanzisha mfuko wa kitaifa wa mpito wa utoaji mdogo wa kaboni na kukuza nishati ya hidrojeni, nishati ya kijani na mambo mengine mapya yanayoweza kuleta ongezeko.

Mali za ardhi na nyumba: Kudhibiti ongezeko la nyumba mpya, kupunguza akiba ya ardhi na nyumba, na kuboresha mfumo wa utoaji wa ardhi na nyumba na kukidhi mahitaji mbalimbali ya nyumba za kuishi, na kutafuta njia nyingi zaidi za kuboresha hali ya uuzaji wa nyumba za kibiashara

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha