Lugha Nyingine
Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China lafanya kikao cha tatu cha wajumbe wote

Kikao cha tatu cha wajumbe wote wa mkutano wa nne wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 8, 2026. (Xinhua/Cao Yiming)
BEIJING - Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), chombo kikuu cha ushauri wa kisiasa cha China, imefanya kikao cha tatu cha wajumbe wote wa mkutano wa nne wa mwaka unaoendelea mjini Beijing jana Jumapili.
Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya CPPCC, alihudhuria kikao hicho.
Maofisa waandamizi kutoka Kamati Kuu ya CPC na Baraza la Serikali la China walialikwa kwenye kikao hicho.
Kwenye kikao hicho, wajumbe 14 wa baraza hilo walitoa maoni yao juu ya mada mbalimbali.
Lian Yimin amesisitiza umuhimu wa kusukuma mbele maendeleo ya miji na vijiji kwa mpango wa jumla na uratibu ili kupiga hatua madhubuti kuelekea kufikia ustawi wa pamoja kwa watu wote.
Chen Xingying amesema kwamba mustakabali wa Taiwan uko katika muungano wa China. Ametoa wito wa kufanya juhudi za pamoja ili kulinda maendeleo ya amani ya jumla ya uhusiano wa pande mbili za Mlango Bahari wa Taiwan na kuhimiza maendeleo yanayofungamana katika pande za Mlango Bahari.
Sze Wing-wai amesema ni muhimu sana kuimarisha msingi wa "nchi moja, mifumo miwili," kuinua kiwango cha usimamizi wa jamii, na kushughulikia matatizo yanayofuatiliwa na watu.
Panchen Erdeni Chos-kyi rGyal-po amesema kwamba ustawi na utulivu wa nchi unatoa uhakikisho wa kimsingi kwa maendeleo mazuri ya dini. Ameongeza kwamba, jamii ya dini ya Kibudha ya Kitibet itajifungamana kwa hiari zaidi na maendeleo ya jumla ya nchi.
Ilzat Ahmatjan ametoa wito wa kufanya juhudi za kuongeza mchangamano, mawasiliano na mafungamano ya makabila yote na kuendeleza zaidi jumuiya ya taifa la China.
Wang Jinnan amesisitiza ni lazima kuharakisha kazi ya kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii yasiyoleta uchafuzi na ya utoaji kaboni chache, kueneza njia ya kuishi maisha katika hali ya kupatana na mazingira, na kusukuma mbele ujenzi wa China Inayopendeza.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma