Wang Yi asema uwepo wa ncha nyingi ndivyo mazingira ya kimataifa yanavyopaswa kuwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 09, 2026

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kwamba utofauti ni asili inayorithiwa ya jamii ya binadamu, na uwepo wa dunia ya ncha nyingi ndivyo mazingira ya kimataifa yanavyopaswa kuonekana.

Wang ametoa kauli hiyo jana Jumapili wakati akijibu swali kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani kwenye mkutano na waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano unaoendelea wa Bunge la Umma la China.

“China na Marekani bila shaka zina mshawishi mkubwa kwa dunia, lakini kuna nchi zaidi ya 190 kwenye sayari hii. Mustakabali wa binadamu wakati wote umekuwa ukijengwa kupitia juhudi za pamoja za mataifa yote." Wang amesema

"China kamwe haitachukua njia ya kutafuta umwamba kadri nguvu yake inavyozidi kuongezeka, wala hatukubaliani na mantiki kwamba dunia inaweza kuendeshwa na nchi kubwa," Wang amesema, akiongeza kuwa China imejitolea kufuata njia ya maendeleo ya amani.

Kuhusu jinsi mazingira ya kimataifa yanavyopaswa kubadilika, Wang amesema pendekezo la China ni kujenga Dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu.

"Hili linapaswa kuwa jukumu la pamoja la nchi zote." Ameongeza.

Alisema kwa rasilimali na uwezo zaidi, nchi kubwa zinapaswa kuwa zenye ukarimu zaidi, kubeba majukumu zaidi, na kuweka mfano wa kuigwa kwa kuzingatia sheria, kuheshimu ahadi na kushikilia sheria za kimataifa.

"China itaendelea kubeba jukumu la kiujenzi katika dunia inayoendelea kubadilika na kufanya kazi na nchi zote kuelekea dunia ya ncha nyingi," ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha