Jeshi la IRGC nchini Iran laahidi utii kwa Kiongozi Mkuu mpya Mojtaba Khamenei

(CRI Online) Machi 09, 2026

Baraza la Wataalamu la Iran limemtangaza mtoto wa Kiongozi Mkuu wa zamani Ali Khamenei, Mojtaba Khamenei, kuwa amechaguliwa kuwa kiongozi mkuu mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika taarifa yake jana Jumapili, baraza hilo limethibitisha kuchaguliwa kwa Mojtaba Khamenei kuwa kiongozi mkuu wa tatu wa nchi hiyo, likirejelea "kura muhimu za wawakilishi waheshimiwa" wa baraza hilo.

Kufuatia tangazo hilo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) mara moja limeahidi utii kwa kiongozi huyo mkuu mpya, likielezea utayari wake wa kufuata amri zake.

Mojtaba Khamenei, aliyezaliwa mwaka 1969, ni mtoto wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei, ambaye aliuawa katika mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israeli. Israeli na Marekani zote zimetoa vitisho kwa Iran kuhusu hatua hii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha