Mashambulizi ya droni kwenye masoko mawili nchini Sudan yaua watu 40 na kujeruhi wengine 59

(CRI Online) Machi 09, 2026

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari na mashuhuda katika Jimbo la Kordofan Magharibi nchini Sudan, mashambulizi ya droni kwenye masoko mawili mjini Abu Zabad na Wad Banda yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 40 na wengine 59 kujeruhiwa siku ya Jumamosi.

Chanzo cha habari kutoka hospitali katika mji huo wa Abu Zabad kimesema kwamba soko moja mjini humo lilishambuliwa na droni Jumamosi. Kimesema kuwa, Hospitali Kuu ya Abu Zabad, ambayo ni idara pekee ya matibabu inayoendelea kutoa huduma za matibabu mjini humo, imepokea miili ya waathirika takriban 24 na majeruhi 31.

Wakati huohuo, shuhuda kutoka mji wa Wad Banda, umbali wa kilomita takriban 16 magharibi mwa Abu Zabad, amesema droni moja ilishambulia soko kuu la mji huo Jumamosi, na kusababisha vifo vya raia 16 huku wengine 28 wakijeruhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha