Lugha Nyingine
Uganda yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa gwaride la askari wanawake
Uganda imefanya gwaride la askari wanawake pekee jana Jumapili katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ambayo imeadhimishwa kitaifa chini ya kaulimbiu ya "Kuongeza Uwekezaji ili kuharakisha upatikanaji wa haki kwa wanawake na mabinti nchini Uganda.”
Katika hotuba ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni iliyosomwa na Makamu wa Rais Jessica Alupo kwenye gwaride hilo, Rais Museveni amesema Siku ya Wanawake Duniani inatoa fursa kuonyesha nafasi muhimu ya wanawake na mabinti katika maendeleo ya jamii na taifa.
Amesema serikali ya Uganda imekuwa ikihimiza uwezeshaji wa wanawake na mabinti kwa muda mrefu kupitia elimu, sera rafiki na miradi ya kiuchumi ili kuwezesha mchango wao kamili katika maendeleo ya taifa.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma