Lugha Nyingine
Tamasha la filamu la China laanza nchini Madagascar ili kuhimizaa mabadilishano ya kiutamaduni
Madagascar imezindua Tamasha la Filamu la China mwaka 2026 jana Jumapili katika mji mkuu Antananarivo, huku wageni karibu 100 wakihudhuria hafla ya ufunguzi.
Katika hafla hiyo, katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano na utamaduni ya Madagascar Bw. Miary Rasolofoarijaona alitoa shukrani zake za dhati kwa kuandaliwa kwa tamasha hilo kubwa linalofanyika kama sehemu ya shughuli za kusherehekea Mwaka wa mabadilishano ya utamaduni kati ya watu wa China na Afrika.
Amesema tamasha hilo litawezesha watu wa Madagascar kuona utajiri, usasa na kina cha utamaduni wa China.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Madagaska Ji Ping amesema kuzidisha mabadilishano baina ya watu na ya kiutamaduni kati ya China na Afrika kunabeba umuhimu wa kimfano unaozidi mfumo wa pande mbili, hasa katika muktadha wa sasa wa kimataifa uliogubikwa na mgawanyiko kutokana na migogoro ya siasa za kijiografia.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma