Bunge la Umma la China launga mkono mageuzi na maendeleo kupitia utungaji wa sheria bora

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2026

BEIJING – Ripoti iliyotolewa jana Jumatatu kuhusu Kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC), ambacho ni chombo cha juu cha utungaji wa sheria cha China, inaonesha kuwa, kamati hiyo ilihudumia na kuunga mkono mageuzi na maendeleo kwa kupitia utungaji wa sheria wa sifa bora katika mwaka uliopita.

Ripoti hiyo ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China iliwasilishwa jana Jumatatu kwenye mkutano wa nne bunge hilo la umma ili ithibitishwe.

Ripoti hiyo inasema kuwa, katika mwaka 2025 uliopita, Kamati hiyo iliimarisha utekelezaji wa Katiba ya Nchi na usimamizi unaofuata kanuni, na kuhakikisha utawala wa kufuata sheria una umoja.

Katika mwaka uliopita, bunge hilo la umma lilithibitisha miswada ya sheria, ufafanuzi wa sheria na maamuzi ya sheria 40 na kupitisha 24 kati yake, ikiwa ni pamoja na sheria sita mpya, sheria 14 zilizofanyiwa marekebisho, ufafanuzi mmoja wa sheria, pamoja na maamuzi matatu kuhusu mambo ya sheria na masuala mengine makubwa. Pia lilifanya maamuzi juu ya kuidhinishwa kwa mikataba tisa na makubaliano muhimu.

Ripoti hiyo imesema, katika kuimarisha utungaji wa sheria kuhusu uchumi, Kamati hiyo ilitunga "Sheria ya Kuhimiza Maendeleo ya Uchumi wa Kibinafsi" mwaka jana, na kuweka bayana kanuni za utendeaji wa usawa, ushindiani wa usawa, ulinzi wa usawa, na kutafuta maendeleo kwa pamoja.

Kamati hiyo iliifanyia marekebisho Sheria ya Ushindani Usio wa Haki, sheria ambayo ina umuhimu wake mkubwa katika kuendeleza uchumi wa fedha wenye uhusiano na uaminifu chini ya utekelezaji wa sheria, na wakati huo huo ilizifanyia marekebisho Sheria ya Biashara Baharini, Sheria ya Utoaji Hukumu, na Sheria ya Biashara ya Nje ili kuendana zaidi na sheria za kimataifa, na hivyo kuhudumia vizuri zaidi ufunguaji mlango wa kiwango cha juu.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa, katika kuhimiza utungaji wa sheria kuhusu usimamizi wa jamii na ustawi wa umma, bunge hilo la umma lilitangaza hadharani "Sheria ya Kukabiliana na Dharura ya Afya ya Umma" na kuifanyia marekebisho "Sheria ya Kinga na Matibabu ya Magonjwa ya Kuambukiza".

Inasema kuwa, katika kuimarisha utungaji wa sheria kuhusu usalama wa nchi na umma, Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge la Umma ilitunga "Sheria ya Nishati ya Atomiki" ili kuunga mkono utafiti, maendeleo, na matumizi ya amani ya nishati ya atomiki kwa mujibu wa sheria, na kuifanyia marekebisho "Sheria ya Usalama wa Mtandao wa Intaneti" ili kuongeza usalama wa data na ulinzi wa taarifa binafsi.

Ripoti hiyo pia imetangaza mpango wa kazi wa bunge hilo la umma katika mwaka 2026. Imeeleza kuwa, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma itahimiza utekelezaji wa pande zote wa Katiba ya Nchi na kukamilisha mfumo wa sheria wa ujamaa wenye umaalum wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha