Lugha Nyingine
Bunge la Umma la China lafanya kikao cha pili cha wajumbe wote

Kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 9, 2026. (Xinhua/Li Tao)
BEIJING – Mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), chombo cha juu cha utungaji sheria cha China, umefanya kikao chake cha pili cha wajumbe wote jana Jumatatu.
Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama na serikali, wakiwemo Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng, walihudhuria kikao hicho.
Zhao Leji, mwenyekiti wa Bunge la Umma la China alitoa ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya bunge hilo la umma kwenye kikao hicho.
Zhao akisema kuwa maendeleo mapya yamepatikana katika kazi mbalimbali mwaka 2025, amesisitiza juhudi za kamati hiyo katika kukamilisha mfumo wa utawala wa kisheria wa ujamaa wenye umaalum wa China na katika kujenga nchi ya kijamaa chini ya utawala wa kisheria katika kiwango cha juu zaidi.
Kwa kutupia macho siku za baadaye, Zhao amesema kamati hiyo itahimiza kazi yake kwa hatua madhubuti, kusukuma mbele maendeleo yenye sifa bora ya kazi ya bunge la umma, na kutoa mchango unaotakiwa kwa ajili ya mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China (2026-2030). Katika ripoti yake hiyo pia ameelezea kazi muhimu ya kamati hiyo katika mwaka huu.
Mkuu wa Mahakama Kuu ya Umma ya China (SPC) Zhang Jun alipotoa ripoti kuhusu mahakama kuu hiyo alisema katika mwaka 2025 mahakama hiyo iliweka mkazo katika kazi ya kutoa huduma za mahakama za sifa bora ili kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Zhang amesema, katika mwaka 2026, mahakama za China zitatilia maanani zaidi katika kulinda na kuhimiza haki na usawa kwenye jamii, na kuimarisha kazi ya kusikiliza na kushughulikia kesi ili kutoa huduma na uhakikisho vyenye nguvu ya kimahakama kwa ajili ya mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano.
Mkuu wa Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China Ying Yong alipotoa ripoti ya kazi ya idara hiyo alisema kwamba katika mwaka uliopita, idara hiyo ilifanya juhudi zaidi za kuhakikisha kila kesi inashughulikiwa kwa sifa bora na ufanisi mzuri zaidi, na kazi ya idara hiyo imepata matokeo mapya.
"Katika mwaka 2026, idara za uendeshaji mashtaka zitaongeza juhudi za kulinda na kuhimiza haki na usawa kwenye jamii, na kutekeleza majukumu na wajibu wa idara hizo ambazo ni vyombo vya nchi vya kufanya usimamizi wa kisheria," Ying amesema.
Ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma kuhusu kazi ya marekebisho ya sheria pamoja na hali ya kushughulikia sehemu fulani ya sheria na maamuzi imewasilishwa kwenye kikao hicho cha Jumatatu ili ithibitishwe.

Zhao Leji, mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, akitoa ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China kwenye kikao cha pili cha wajumbe wote wa mkutano wa nne wa Bunge la Umma la China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 9, 2026. (Xinhua/Rao Aimin)

Zhang Jun, mkuu wa Mahakama Kuu ya Umma ya China (SPC), akitoa ripoti ya kazi ya Mahama hiyo kwenye kikao cha pili cha wajumbe wote wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 9, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Mkuu wa Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China (SPP) Ying Yong akitoa ripoti ya kazi ya Idara hiyo kwenye kikao cha pili cha wajumbe wote wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 9, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Li Hongzhong akiongoza kikao cha pili cha wajumbe wote wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 9, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma