Lugha Nyingine
Erdogan aapa kuiweka Uturuki nje mgogoro wa kikanda, aionya Iran dhidi ya "hatua za kichochezi"
ANKARA - Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kwamba Uturuki inadumisha kiwango cha juu cha kuwa macho wakati huu ambapo kuna mivutano inayozidi kupamba moto ya kikanda, akionya kwamba "hatua za kichochezi" zinaweza kuharibu uhusiano kati ya Ankara na Tehran.
Akizungumza jana Jumatatu baada ya kikao cha baraza la mawaziri mjini Ankara, Rais Erdogan amesema taasisi zote husika zinafanya kazi kwa uratibu na zinaendelea kuwa katika tahadhari katika kukabiliana na mazingira ya usalama yanayoendelea kubadilika. Ameongeza kuwa lengo kuu la serikali ni kuilinda nchi kutoka kwenye machafuko yanayoendelea katika eneo hilo.
Kauli hizo zilikuja baada ya kombora lililorushwa kutoka Iran kuzuiliwa juu ya jimbo la kusini mashariki mwa Uturuki la Gaziantep mapema Jumatatu. Kombora hilo la balestiki, ambalo liliingia katika anga ya Uturuki, liliharibiwa na vifaa vya ulinzi wa anga na makombora vya NATO vilivyofungwa katika eneo la Mashariki la Bahari ya Mediterania. Wizara ilithibitisha kwamba hakukuwa na vifo au majeruhi.
"Tunafuatilia kwa karibu hali zote zinazoendelea tukiwa pamoja na timu zetu zenye uzoefu. Hatutauangusha ulinzi wetu. Lengo letu ni kuiweka nchi yetu mbali kutoka kwenye moto huu," amesema.
Rais huyo amesema kwamba Uturuki imeshatoa tahadhari inayohitajika kwa Iran, lakini "hatua za makosa" ziliendelea kuchukuliwa licha ya tahadhari hizo.
"Licha ya tahadhari zetu, hatua zenye makosa na za kichochezi ambazo zinaweza kuharibu urafiki wa Uturuki zinaendelea kuchukuliwa. Hakuna yeyote anayepaswa kuchukua hatua ambayo inaweka kivuli juu ya uhusiano wetu wa ujirani na undugu wa miaka elfu na kuacha majeraha ya kina katika mioyo na akili za taifa letu." Erdogan amesema.
"Katika muktadha wa tukio la leo (jana Jumatatu), ninakumbusha tena kwamba hakupaswi kuwa na ukaidi katika kuendelea na makosa." amesema.
Ameongeza kuwa anga ya Uturuki ilikuwa ikifuatiliwa saa zote dhidi ya vitisho vinavyoweza kutokea.
"Ndege zetu za kivita za F-16, ndege zetu za kutoa tahadhari mapema angani na ndege za kubeba matanki ya mafuta zinaangalia anga yetu saa zote dhidi ya vitisho vinavyowezekana," amesema.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma