Lugha Nyingine
Tanzania kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na mvua kubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Ashatu Kijaji ametangaza kuwa Tanzania itatenga shilingi bilioni 8.1 za Tanzania (dola za Marekani karibu milioni 3.2) kukarabati barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua kubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Hayo ameyasema Jumapili jioni wakati wa ziara ya ukaguzi wa hifadhi hiyo, ambapo alitathmini uharibifu uliosababishwa na mvua kubwa za hivi karibuni zinazohusiana na mabadiliko ya tabianchi, ambazo zimesababisha magari kadhaa ya watalii kukwama kwa muda mrefu.
Kijaji amesema serikali itatoa fedha hizo haraka ili kuhakikisha ukarabati wa miundombinu iliyoathiriwa unafanywa kwa wakati, ikiwa ni pamoja na madaraja na barabara muhimu kwa shughuli za utalii katika hifadhi hiyo.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma