Lugha Nyingine
China yachangia dola za kimarekani milioni 2 kusaidia Wasomali walioathiriwa na ukame
China imechangia dola za kimarekani milioni 2 ili kusaidia jamii zilizoathiriwa na ukame unaoendelea kote nchini Somalia, ambapo karibu watu milioni 6.5 wanakadiriwa kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Balozi wa China nchini Somalia Bw. Wang Yu amekabidhi mchango huo juzi Jumapili kwa Shirika la Usimamizi wa Maafa la Somalia (SoDMA), na kuahidi kuunga mkono juhudi za serikali ya Somalia za kukabiliana na ukame.
Pia amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, hasa katika misaada ya kibinadamu na maendeleo ya kijamii.
Kamishna wa SoDMA Bw. Mohamud Moallim Abdulle ameishukuru China kwa uungaji mkono huo, akisema utasaidia wilaya 72 zilizoathiriwa na ukame, zikiwemo 45 zinazokabiliwa na hali mbaya ya dharura.

Sikukuu ya Jadi ya Taa ya China yasherehekea mkoani Zhejiang

Kupatwa kwa mwezi kikamilifu kwashuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini China

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma