Lugha Nyingine
Wajumbe wa jeshi wajadili hotuba ya Rais Xi kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China

Picha hii iliyopigwa Machi 9, 2026 ikionyesha Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya kikao cha pili cha wajumbe wote cha mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) mjini Beijing. (Xinhua/Jin Liwang)
BEIJING - Wajumbe wa jeshi wanaohudhuria mkutano wa mwaka unaoendelea wa Bunge la Umma la China wamesoma na kujadili hotuba ya Rais Xi Jinping iliyotolewa kwenye kikao cha wajumbe wote cha ujumbe huo, Zhang Xiaogang, msemaji wa wajumbe hao wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano huo wa mwaka wa Bunge amesema Jumanne.
Zhang amesema hotuba hiyo ya Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), imeongeza zaidi na kukuza mwongozo na sera za kuongeza utii wa kisiasa katika jeshi.
Wakati akihudhuria kikao hicho siku ya Jumamosi wiki iliyopita, Rais Xi alisisitiza kutumia vya kutosha na nguvu bora ya kipekee ya kuongeza utiifu wa kisiasa wa jeshi, na alitoa wito wa kufanya juhudi za pamoja kwa moyo mmoja, na kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa katika ulinzi wa taifa na ujenzi wa jeshi kwa hatua madhubuti na endelevu.
Zhang amesema wajumbe wa jeshi wameahidi kutekeleza utaratibu wa uongozi wa hakika wa mwenyekiti wa CMC, kuendelea kuzidisha marekebisho ya kisiasa, kuimarisha mafunzo ya kijeshi na maandalizi ya kupigana vita kwa pande zote, na kuunganisha nguvu ili kusukuma mbele maendeleo yenye sifa bora.
Kuhusu bajeti ya ulinzi wa nchi, kiasi kilichotengwa kwa ulinzi wa taifa kutoka kwenye bajeti ya umma ya kitaifa ya mwaka 2026 kinakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 6.9 kuliko matumizi halisi ya mwaka uliopita. Kati ya kiasi hicho, matumizi ya serikali kuu kwa ulinzi wa taifa yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 7.
Zhang ametaja maeneo manne ya kupewa kipaumbele katika ongezeko hilo la bajeti ya ulinzi kwa mwaka huu: Kwanza; kuhimiza maendeleo jumuishi ya vikosi vyote vya jeshi kupitia maendeleo ya mashine za kijeshi, upashanaji habari, na matumizi ya teknolojia za kisasa, pili; kuboresha mfumo wa kufanya operesheni ya pamoja na kuongeza ujenzi wa uwezo wa hali ya juu wa kupigana vita, tatu; kuharakisha maendeleo ya uvumbuzi wa silaha na teknolojia za hali ya juu za ulinzi wa nchi, kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya ugavi ya kisasa, na nne; kuongeza marekebisho ya kisiasa na kuhimiza mafunzo ya kijeshi chini ya hali halisi ya kupigana vita.
Kuhusu "nguvu ya kutaka Taiwan ijitenge," Zhang amesema jeshi la China litapambana kithabiti na nguvu ya mafarakano ya kutafuta "kujitenga kwa Taiwan" na kupinga uingiliaji wa nje.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



