Lugha Nyingine
Tume ya utendaji wa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China yafanya kikao cha pili

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya utendaji wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), akiongoza kikao cha pili cha tume hiyo ya utendaji wa mkutano katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 10, 2026. (Xinhua/Gao Jie)
BEIJING – Tume ya Utendaji wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), imefanya kikao chake cha pili jana Jumanne, kikiongozwa na Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo.
Kikao hicho kimeamua kuwasilisha muswada uliorekebishwa wa sheria ya mazingira, muswada uliorekebishwa wa sheria ya kuhimiza umoja na maendeleo ya makabila, na muswada uliorekebishwa wa sheria ya mpango wa maendeleo ya nchi kwa wajumbe wa Bunge la Umma la China ili wathibitishwe.
Kikao hicho pia kimeamua kuwasilisha nyaraka nyingine za -- Mswada wa azimio la ripoti ya kazi ya serikali; Mswada wa azimio la mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii; Mswada wa azimio ya ripoti ya mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi na mpango wa mwaka 2026; na Mswada wa ripoti ya bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa na bajeti za mwaka 2026 -- kwa wajumbe wa Bunge la Umma la China ili wathibitishwe.
Zhao, ambaye pia ni mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, aliongoza kikao cha wenyeviti watendaji wa tume ya utendaji wa mkutano kabla ya kikao hicho cha pili cha tume ya utendaji wa mkutano.

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya utendaji wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), na mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, akiongoza kikao cha kwanza cha wenyeviti watendaji wa kamati ya utendaji katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 10, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



