Wajumbe wa mkutano wa Bunge la Umma la China wawasilisha mapendekezo 226 kwenye mkutano wa mwaka wa bunge hilo la umma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 11, 2026

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye sekretarieti ya mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) mjini Beijing, Machi 10, 2026. (Xinhua/Wang Xi)

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye sekretarieti ya mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) mjini Beijing, Machi 10, 2026. (Xinhua/Wang Xi)

BEIJING – Wajumbe wa Mkutano wa Bunge la Umma la China wamewasilisha mapendekezo 226 kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China hadi kufikia Jumapili adhuhuri, ambayo ilikuwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha mapendekezo kwenye mkutano huo wa nne wa Bunge hilo la Umma unaoendelea mjini Beijing.

Sekretarieti ya mkutano huo wa mwaka wa Bunge hilo la Umma imesema jana Jumanne kwamba pia imepokea mapendekezo zaidi ya 7,000 kutoka kwa wajumbe wa Bunge la 14 la Umma la China. Imesema, mapendekezo hayo mengi yanahusu kazi ya kutunga sheria.

Sekretarieti hiyo imesema, mapendekezo hayo yanahusu mada nyingi mbalimbali, kama vile kuendeleza soko la pamoja la kitaifa, kukuza vichocheo vipya vya ukuaji, na kuharakisha kujitegemea na kujiimarisha katika sekta ya sayansi na teknolojia ya kiwango cha juu.

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye sekretarieti ya mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) mjini Beijing, Machi 10, 2026. (Xinhua/Wang Xi)

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye sekretarieti ya mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) mjini Beijing, Machi 10, 2026. (Xinhua/Wang Xi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha