Raia zaidi ya 1,300 waripotiwa kuuawa, maeneo karibu 10,000 ya kiraia yaharibiwa nchini Iran

(CRI Online) Machi 11, 2026

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani amesema Jumanne kuwa raia zaidi ya 1,300 wameuawa na maeneo 9,669 ya kiraia yameharibiwa nchini Iran katika mashambulizi ya kijeshi yaliyoanzishwa na Marekani na Israeli tangu Februari 28.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Iravani amesema maeneo ya kiraia ni pamoja na nyumba 7,943 za makazi, vituo 1,617 vya biashara na huduma, vituo 32 vya matibabu na dawa, shule na taasisi 65 za elimu, majengo 13 ya Hilali Nyekundu, na vituo kadhaa vya usambazaji wa mafuta.

“Wanalenga kwa makusudi na kiholela raia na miundombinu ya kiraia kote katika nchi yangu. Hawaoneshi heshimu kwa sheria za kimataifa na wala hawajizuii katika kufanya uhalifu huu.” Amesema.

Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua sasa ili kukomesha vita hivyo vya umwagaji damu dhidi ya watu wa Iran.

“Tutatachukua hatua zote za lazima kulinda watu wetu, ardhi yetu, na uhuru wetu” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha