Lugha Nyingine
Mkutano wa biashara Afrika wahimiza mafungamano imara zaidi ya kikanda ili kukuza biashara ya ndani ya Afrika
Watunga sera na viongozi wa biashara wa Afrika wametoa wito wa mafungamano imara zaidi ya kikanda na kuondoa vizuizi vya kibiashara ili kukuza biashara ya ndani ya bara la Afrika kwenye Mkutano wa Biashara wa Afrika 2026 uliofanyika Cape Town, Afrika Kusini jana Jumatano.
Mkutano huo wa siku moja, uliofanyika chini ya kaulimbiu ya “Kubadilisha Dira Kuwa Kasi: Kujenga Mfumo Ikolojia wa Biashara wa Afrika Kwa Mchango Halisi Duniani”, uliwaleta pamoja watunga sera, taasisi za maendeleo, viongozi wa biashara na wawekezaji ili kujadili njia za kuharakisha ushiriki wa Afrika katika biashara ya dunia wakati ikipanua biashara ya ndani ya bara.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kanda ya Kusini mwa Afrika, Kennedy Mbekeani amesema maendeleo ya dunia katika miaka ya karibuni yamekuwa yakionesha hitaji la Afrika katika kuimarisha mafungamano ya kikanda.
Akiongea kwenye mjadala wa wanajopo katika mkutano huo, Waziri wa Biashara na Ujasiriamali wa Botswana, Tiroeaone Ntsima amesema nchi za Afrika zinaweza kunufaika kutokana na ufunguaji wa mipaka na ufadhili wa pamoja wa miradi ya kuvuka mipaka.
Amesisitiza haja ya kuimarisha uratibu kati ya nchi majirani, akisema njia ya biashara na taratibu za kuvuka mipaka zinatakiwa kurahisishwa ili kutoa urahisi kwa kampuni na watu binafsi kusafirisha bidhaa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



