Lugha Nyingine
Tanzania yatoa tahadhari dhidi ya kuvuka barabara zilizofurika maji katika Hifadhi ya Serengeti
Jumuiya ya Waendesha Shughuli za Utalii Tanzania (TATO) imetoa taarifa ya dharura kwa umma ikiwahimiza wadau wa sekta ya utalii kuepuka kuvuka mito na barabara zilizofurika maji katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wakati huu ambapo mafuriko makubwa yamesomba magari kadhaa na kuzua hali ya wasiwasi kuhusu watu ambao hawajulikani walipo.
TATO imesema kuwa mvua kubwa imesababisha mafuriko katika maeneo ya Serengeti na kuleta mazingira hatari kwa waendesha biashara ya utalii, waongoza watalii, na watalii wanaosafiri katika Hifadhi hiyo.
Katika taaarifa hiyo, mwenyekiti wa jumuiya hiyo Wilbard Chambulo ameshauri wadau husika wa utalii kurudi walikotoka wanapokuta barabara zilizofurika, kusubiri viwango vya maji kupungua, au kuwasiliana na nyumba za kulala wageni na waendeshaji huduma wengine ili kutafuta njia mbadala salama za usafiri.
Jumuiya hiyo, pia imewasihi wadau wa biashara hiyo ya utalii kueneza mara moja taarifa ya usalama kwa timu zinazofanya operesheni katika Hifadhi ya Serengeti ili kuepusha ajali zinazoweza kutokea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



