Lugha Nyingine
Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China lamaliza mkutano wa mwaka

Mkutano wa nne wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) ukifanya kikao chake cha kufungwa kwa mkutano wa mwaka katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 11, 2026. (Xinhua/Yan Yan)
BEIJING - Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambayo ni chombo cha juu cha ushauri wa kisiasa cha China, imemaliza mkutano wake wa mwaka jana Jumatano asubuhi.
Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama na serikali ya China, wakiwemo Li Qiang, Zhao Leji, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng, walihudhuria kikao hicho cha kufungwa kwa mkutano wa mwaka katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Akiongoza kikao hicho, Wang Huning, mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China amesema mkutano wa mwaka wa chombo hicho cha juu cha mashauriano ya kisiasa umepata matokeo kemkem.
Amesema, wajumbe wa baraza hilo wanaotoka sekta zote mbalimbali wameongeza zaidi imani yao ya kutoa mchango kwa ajili ya kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na kudumisha ukuaji wa haraka wa uchumi wa China na utulivu wa jamii wa muda mrefu.
Wang amesema kuwa mwaka 2026 ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China ni lazima lishikilie uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), lioneshe umuhimu wake wa kuwa jumuiya ya kisiasa, lifanye juhudi za kutoa maoni na mapendekezo, na liunganishe nguvu na hekima ili kuhakikisha mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Mpango huo wa 15 wa Miaka Mitano.
Wang ametoa wito wa kuwataka wajumbe wa baraza hilo kutoa mapendekezo zaidi ya kuchangia ustawi wa umma, kufanya mambo mengi ya kivitendo yanayoleta manufaa kwa maisha ya watu, na kusaidia kuyafanya matunda ya ujenzi wa mambo ya kisasa yanufaishe wananchi wote.
Amesema baraza hilo linapaswa kusaidia kukusanya nguvu chanya ya watu wa China ndani na nje ya nchi ili waweze kusonga mbele katika safari mpya na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa zama mpya.
Mkutano huo umepitisha azimio ya ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, azimio ya ripoti kuhusu hali ya kushughulikiwa kwa mapendekezo ya wajumbe wa baraza hilo tangu mkutano wa tatu wa mwaka uliopita, ripoti ya uthibitishaji wa mapendekezo mapya, na azimio la kisiasa la mkutano wa nne wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China.

Wang Huning, mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akiongoza kikao cha kufungwa kwa mkutano wa nne wa baraza hilo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 11, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

Kikao cha kufungwa kwa mkutano wa nne wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 11, 2026. (Xinhua/Chen Yehua)

Kikao cha kufungwa kwa mkutano wa nne wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 11, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Kikao cha kufungwa kwa mkutano wa nne wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 11, 2026. (Xinhua/Yao Dawei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



