Tume ya Utendaji wa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China yafanya kikao cha tatu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2026

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya utendaji  wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), akiongoza kikao cha tatu cha tume hiyo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2026. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING – Tume ya utendaji wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), imefanya kikao chake cha tatu jana Jumatano.

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo ya utendaji, aliongoza kikao hicho.

Kikao hicho kimeamua kuwasilisha mswada wa sheria ya mazingira, mswada wa sheria ya kuhimiza umoja na maendeleo ya makabila, na mswada wa sheria ya mipango ya maendeleo ya kitaifa kwa kupigwa kura kwenye kikao cha wajumbe wote cha mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China.

Kikao hicho kimeamua kuwasilisha nyaraka nne kwa kuthibitishwa na wajumbe wa Bunge la Umma la China. Nyaraka hizo ni muswada wa maazimio juu ya ripoti za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China, pamoja na muswada wa uamuzi juu ya kuidhinisha ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China kuhusu kazi ya marekebisho ya sheria na mapendekezo ya kushughulikia sheria husika na maamuzi husika.

Kikao hicho pia kimesikiliza na kupitisha ripoti kuhusu kazi ya kushughulikia mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wa Bunge la Umma la China wakati wa mkutano wa nne mwaka wa bunge hilo.

Zhao, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, aliongoza kikao cha wenyeviti watendaji wa tume ya utendaji wa mkutano kabla ya kikao chake hicho cha tatu.

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya utendaji wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) na mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge hilo la Umma, akiongoza kikao cha pili cha wenyeviti watendaji wa tume hiyo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha