Trump atuma ujumbe mbalimbali unaochanganya juu ya lini mashambulizi dhidi ya Iran yataisha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2026

Watu wakihudhuria maandamano kupinga mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran mjini San Francisco, Marekani, Februari 28, 2026. (Picha na Ziyu Julian Zhu/Xinhua)

Watu wakihudhuria maandamano kupinga mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran mjini San Francisco, Marekani, Februari 28, 2026. (Picha na Ziyu Julian Zhu/Xinhua)

WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Iran ni vita na pia "operesheni" ya muda mfupi, akituma ujumbe mbalimbali unaochanganya juu ya lini mashambulizi hayo yataisha.

"Umesema punde tu kuwa ni operesheni ndogo na umesema ni vita. Kwa hivyo, ni nini hasa?" Trump aliulizwa na mmoja wa waandishi wa habari waliokuwa wakisafiri naye katika Jimbo la Ohio la Marekani jana Jumatano.

"Naam, ni vyote viwili. Ni operesheni ambayo itatuweka nje ya vita, na kwa vita itakuwa, ninamaanisha kwa wao ni vita." Trump amejibu.

Akihutubia Wabunge wa Chama cha Republican siku ya Jumatatu, Trump aliielezea operesheni hiyo ya kijeshi dhidi ya Iran kuwa ni "operesheni ya muda mfupi" wakati huohuo baadaye akiapa "kusonga mbele kwa kudhamira zaidi kuliko hapo awali ili kupata ushindi wa mwisho." Pia ametaka "kujisalimisha bila masharti kwa Iran."

Hata hivyo Trump alisema mapema siku hiyo ya Jumatano kwamba vita hivyo vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vitaisha "hivi karibuni" kwa sababu "hakuna chochote kilichobaki cha kulengwa," chombo cha habari cha Axios kimeripoti.

Maafisa wa Marekani na Israel wamesema kwamba wanajiandaa kwa angalau wiki mbili zaidi za mashambulizi nchini Iran, na kwamba hakujawa na maelekezo ya ndani kuhusu ni lini mashambulizi ya namna hayo yanaweza kusimama, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Raia zaidi ya 1,300 wameshauawa na maeneo 9,669 ya kiraia yameharibiwa nchini Iran katika mashambulizi hayo ya Marekani na Israel tangu Februari 28, Amir Saeid Iravani, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, alisema juzi Jumanne.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha