Rais wa Iran aorodhesha masharti ya kumaliza vita na Marekani na Israel

(CRI Online) Machi 12, 2026

Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kwamba njia pekee ya kumaliza vita vyake na Marekani na Israel ni kutambua haki halali za Iran, ulipaji wa fidia, na mahakikisho thabiti ya kimataifa dhidi ya uchokozi wa siku za baadaye.

Katika ujumbe wake aliouchapisha kwenye mtandao wa X jana Jumatano, Pezeshkian ameelezea“dhamira ya Iran kwa amani katika eneo hilo ”.

Mapema siku hiyo, vikosi vya jeshi la Iran vilionya kwamba vitaanzisha mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi, kama Marekani itashambulia bandari za Iran.

Awali, kamandi ya mashariki ya kati ya Marekani ilitangaza kwenye ukurasa wake wa Lugha ya kiajemi katika mtando wa kijamii wa X, ikihimiza raia nchini Iran kukaa mbali mara moja na vituo vya bandari ambako vikosi vya majini vya Iran vinafanya shughuli za kijeshi.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha