Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China atoa wito wa kukoma kwa operesheni za kijeshi katika Mashariki ya Kati
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ametoa wito kwa pande zote kuhimiza wale wanaohusika katika mgogoro wa sasa wa Mashariki ya Kati kusimamisha operesheni za kijeshi mapema iwezekanavyo na kuepusha hali kuzorota zaidi.
Wang ametoa wito huo alipofanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Misri, Badr Abdelatty.
Amesisitiza msimamo wa kikanuni wa China, akisema China na Misri, zikiwa nchi zinazowajibika, zote zinatetea kutatua masuala ya kikanda kwa njia ya mazungumzo na mashauriano na zinapinga matumizi ovyo ya nguvu.
Amesema mgogoro wa muda mrefu zaidi katika Mashariki ya Kati utaleta tu mateso na machungu kwa watu wa eneo hilo, kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa kikanda, na kuharibu zaidi usalama na utulivu wa kikanda na kimataifa.
Akisisitiza kuwa usimamishaji vita wa mara moja unawakilisha maafikiano mapana ya jumuiya ya kimataifa, Wang amesema China iko tayari kudumisha mawasiliano na uratibu na nchi za kikanda ikiwemo Misri, na kuendelea kufanya kazi ya kiujenzi kwa ajili ya kurejesha amani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



